MSANII anayefanya tasnia ya filamu nchini Salum Mpoyoka amesema kuwa ameanza
kusambaza fiamu yake mpya iitwayo Mume wa Dunia.
Nyota huyo ambaye awali aliwahi kufanya vema katika ujio wake wa filamu iliyoitwa
'Thank You loveness' amesema alifanya maandalizi mazuri kuhakikisha anatoa ujio
utakaovutia mashabiki wa sanaa.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam jana Mpoyoka alipokuwa akizungumza na
mwandishi wa habari hizi ambapo alisema baada ya kuangalia
mapungufu yaliyojitokeza kipindi cha nyuma katika sanaa ameamua kuja
na kauli mbiu ya Bongo Movie Mpya .
Alisema juhudi zake za sasa kupitia sanaa ni kufanya filamu zenye ubora mkubwa
kuzingatia mapungufu yalifanya sanaa hiyo isisonge mbele kama ilivyo kuwa awali,
na kuwa alijipanga na kutumia wasanii chipukizi kusonga mbele.
"Katika filamu hii nimejikita kuzingatia maadili ya kitanzania
na pia nimetumia weledi mkubwa katika kufanikisha ufanisi ili kuleta
badiliko jipya katika tasnia,"alisema Mpoyoka.
Mpoyoka alisema kuwa ili msanii kujiunga na Bongo Movie Mpya alieleza kuwasiliana
kupitia instagram kwenye akaunti za facebook pamojana youtube.
Nyota huyo aliyecheza awali katika ujio wa Thank You loveness iliyowashirikisha
nyota wengine Mzee Chilo,Mzee Magari, pamoja na Hashim Kambi aliweka wazi kuwa katika'Mume wa Dunia'licha ya kuanza kusambazwa Dar es Salaam, itaanza kusambazwa katika mikoani mingine nchini.
Comments