Skip to main content

Mhandisi Isack Kamwelwe akagua kipande kilichotandikwa reli ya kisasa ya SGR

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe
(katikati) akikagua kipande kilichotandikwa reli ya kisasa ya SGR,
Soga mkoani Pwani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye na kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania,Masanja Kadogosa.

MRADI mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge unaendelea
nchini, Reli hiyo itakayoanzia bandari ya Dar es Salaam hadi mji mkuu wa
Dodoma na baadaye hadi nchi za jirani za Rwanda Burundi na DR Congo
umeanza kutandazwa reli katika eneo la soga mkoani Pwani.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua
rasmi kazi ya utandikaji wa reli ya kisasa ya SGR kwenye eneo la Soga lililopo
mkoani Pwani ambapo reli hiyo inajengwa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kwa
 umbali wa kilomita 300 na  kushuhudiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
 Tanzania Masanja Kadogosa.


Akizindua atua hiyo  mkoani humo Kamwelwe aliwahimiza mainjinia 60 wazalendo
wenye utaalamu na ujuzi wa uhandisi wamepata mafunzo na wamehimizwa
kupata weledi kwa kujifunza vema kupitia mradi huo.


alisema Kampuni ya Yapi Merkezi ya nchini Uturuki imeendelea kufanyaujenzi
wake nchini ambapo kupitia ziara hiyo waziri Kamwelwe alitembelea alitembelea
uzalishaji wa mataruma ya zege kwa ajili ya reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar
es Salaam hadi kwenye kambi kuu ya ujenzi wa mradi huo iliyopo Soga.

"Napenda kuwahasa mainjinia wetu kujifunza kupitia mradi hao vijana hao
60  wazalendo wenye utaalamu na ujuzi wa uhandisi wajifunze kwa weledi mkubwa 
wakiwa na kampuni hiyo ya Uturuki,"alisema Waziri Kamwelwe.


Waziri Kamwelwe alisema kuwa reli hiyo ya kisasa itakuwa ya treni yenye
kasi ya kilomota 160 kwa saa na uendeshaji wake utatumia umeme .

Amefafanua kuwa Serikali iliagiza reli peke yake kutoka nchini Japan ambapo
kiasi cha tani 7,250 ziliingizwa nchini katika kipindi cha wiki mbili
zilizopita ambapo reli hizo zitatumika kujenga reli hiyo ya kisasa ya SGR
kwa ukubwa wa kilomita 60. 
Kupitia mradi huo hadi sasa watanzania wamekuwa wakichangamkia fursa za
 ajira zitokanazo na utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya
Standard Gauge Railway (SGR) Line kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.


"serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli
imeendelea kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuwa miradi
mbali mbali imekuwa ikitekelezwa,"alisema Waziri Kamwelwe.

Ameongeza kuwa reli hiyo itatumia umeme na sio dizeli ambapo TANESCO imepewa
jukumu la kutoa umeme kutoka kwenye gridi ya taifa na kuleta kwenye mfumo wa
reli ya kisasa ya SGR ambapo jumla ya megawati 160 zitahitajika kuendesha reli
hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro. Shirika la Reli Tanzania litakuwa na
jukumu la uhandisi ujenzi, madaraja, mifumo na njia kwa ajili ya kuendesha reli
ya kisasa ya SGR.


Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...