CHINA imefungua milango ya biashara ya mazao ya kilimo, ambapo Tanzania imeombwa kupeleka bidhaa za kilimo zilizoongezwa thamani. Pichani Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE)Edwin Rutagenika . Katika hali hiyo zinahitajika tani 200,000 za mbaazi zilizokobolewa na zisizoko bolewa natena wakati huo, zikihitajika tani 138,000 za tangawizi zilizoongezwa thamani. Hayo yamesemwa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE)Edwin Rutagenika alipo rejea kutoka nchini China. “Nilikuwa nchini China hivi karibuni,China imeridhishwa na bidhaa za kilimo ambapo zinahitajika tani nyingi za mazao mbalimbali ya kilimo,”Alisema Bidhaa za kilimo zilizooledheshwa ni pamoja na korosho,mbaazi,kahawa, tangawizi, mhogo, choroko na kunde. Rutagenika alisema kuwa wana jukumu la kukuhakikisha bidhaa na mazao yan...