Skip to main content

Taarifa iliyotolewa na Serikali baada ya kauli za jana za Tundu Lissu



Serikali imemshauri Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu kutekeleza wajibu wake kwa kusimamia weledi akiwa kama Wakili wa Mahakama Kuu badala ya kufanya Propaganda kwa kutumia lugha ya kejeli, kuudhi na uchochezi kuituhumnu Serikali kuwa inabana demokrasia.
Alieyasema hayo leo ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi katika taarifa kwa Umma aliyoitoa juu ya ufafanuzi kuhusu propaganda na upotoshaji wa Mbunge huyo.
“Vyombo mbalimbali vya habari leo vimemnukuu Mbunge wa Singida Mashariki Ndugu Tundu Lissu ambapo pamoja na mambo mengine, huku wakati fulani akitumia lugha za kuudhi, uchochezi na kejeli, ameituhumu Serikali kuwa inabana demokrasia nchini,” imefafanua taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa madai kwamba Serikali inakandamiza demokrasia ni propaganda tu za kisiasa, kutokana na Lissu kuonekana kuchanganya kati ya haki katika demokrasia ambazo hata yeye amezitumia kuongea na wanahabari bila tashtiti kwa upande mmoja na misingi ya wajibu kwa upande mwingine ambayo kila mmoja, iwe Tanzania au kwingineko duniani, anayo na pale anapoikiuka hatua huchukuliwa.
Dkt. Abbasi amesema kuwa tofauti na upotoshaji wa Lissu, Tanzania ikiwa nchi kiongozi Afrika na duniani katika kuenzi demokrasia na kupigania haki, si tu inaendelea kuenzi misingi hiyo bali pia imechukua hatua za wazi kuhakikisha kuwa misingi hiyo inalindwa na pale mtu na hata taasisi zinapokiuka basi mkondo wa sheria, jambo muhimu katika utawala bora, huchukua nafasi yake

Vilevile ameeleza kuwa, Tanzania ni ikiwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) imeridhia mkataba wa Kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa wa mwaka 1966 na huwasilisha taarifa zake za utekelezaji wa demokrasia na haki za binadamu katika kamisheni ya UN ya haki za binadamu.
Pia ni mwanachama kiongozi wa Umoja wa Afrika (AU) ambapo imeridhia Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu na ni miongoni mwa nchi za kwanza kabisa Afrika kukubali kushtakiwa na wananchi wake kwa kuridhia itifaki ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na pia kukubali kufanyiwa ukaguzi katika utawala bora kupitia Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).
Dr. Abbasi
“Ni kwa sababu hizi basi tunamuasa Ndugu Lissu na wananchi kwa ujumla kujiepusha na propaganda, kejeli na uzushi usio na msingi dhidi ya Serikali au taasisi zake na pale ambapo wanadhani kuna haki zimekiukwa badala ya kuvunja sheria ni vyema kutafuta haki kupitia mkondo wa kisheria ambao tumeuainisha hapo juu,” imefafanua taarifa hiyo.
Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali itaendelea kuenzi na kuilinda misingi ya demokrasia, uhuru wa watu na kuwapa fursa wananchi kushiriki katika uchumi wa nchi hasa wakati huu wa mageuzi makubwa ya kiutendaji chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli lakini haitavumilia mtu yeyote au kikundi chochote kitakachojaribu kutumia uhuru wowote vibaya ili tu kukwaza azma hiyo ya Taifa.

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...

Poland’s GROM special services mastermind found dead

Brigadier General Slawomir Petelicki, responsible for the formation of the GROM special services unit in the 1990s, was found dead at his apartment, Saturday, with bullet wounds to the head. Sławomir Petelicki, 1946-2012. Photo: Archive/PAP/Radek Pietruszka Police spokesman Maciej Karczynski informed that Petelicki’s body was found by his wife in the garage of his Warsaw apartment on Saturday. He was 65. Primary investigations point to suicide as the cause of death. It is expected that prosecutors will decide on an investigation into Petelicki’s death on Monday. After examining the scene of the incident, “the body of General [Petelicki] has been taken to a forensic laboratory, although a post-mortem will probably take place on Monday,” prosecutor Katarzyna Calow-Jaszewska from the Warsaw District Prosecution told the PAP news agency. “He was a tough man, a brilliant soldier and commander,” Colonel Krzysztof Przepiorka, head of the ...