MADIWANI wa Chama cha Wananchi(CUF) jana Dar es Salaam wamekutana katika ofisi zao
na kutoa tamko rasmi juu ya sintofahamu inayoendelea kaika chama hicho.
Kwa pamoja wameunga mkono hotuba na msimamo wa Chama chao uliotolewa
hivi karibuni na Katibu wao Mkuu Maalim Seif Sharifu Hamad, madiwani hao
wa CUF kutoka manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam walitoa ujumbe huo ili
uweze kuwafiki wana chama wao na wapenda mabadiliko nchini kwa ujumla.
Wakizungumza juu ya msimamo wao madiwani hao walisema kuwa chama cho
kilishiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015bila ya kuwa na mwenyekiti
wa Chama Taifa kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wao
Profesa Ibrahim Lipumba kwa utashi wake mwenyewe mbali na kumusihi
sana kusitisha mpango wake huo.
"Kila mmoja wetu kwa upande wao alishiriki kwa namna moja ama nyingine
kuhakikisha Profesa Lipumba hajiuzulu nafasi ya uenyekiti wa chama
Taifa,waliamini kuwa kujiudhulu kwake kungeweza kuleta athari
kwetu tuliamini kuwa kujiuzuru kwake kungeweza kuleta athari
kwa sisi wagombea watarajiwa wakati huo na kuathiri ushirikiano
wa vyama vyetu katika UKAWA,"Alisema Omry Kumbilamoto
ambaye ni naibu mea Ilala.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Omry alisema kuwa Profesa Lipumba alipuuza kilio chao wote wana CUF
ambapo alishikilia msimamo wake na mara baada ya kutoa taarifa
hiyo rasmi ya Kung'atuka ama kujiuzulu pale kwenye hoteli ya Peacock
Augusti 2016 ambapo alielekea Kigali nchini Rwanda kwa shughuli
aliyoiita a utafiti wa kiuchumi wenyelengo la kuja kuisaidia
serikali ijayo ya awamu ya Tano.
Aidha alisema kuwa wao madiwani 19 waliopo mbele kwa wakati huo jana waliweza pia
kupambana katika uchaguzi Mkuu wa Otoba mwaka 2015 bila ya kuwa na Makamu
Mwenyekiti Taifa Mhe. Juma Duni Haji ambaye kwa mujibu wa makubaliano
ya UKAWA alilazimika kujiunga Chadema ili apate nafasi ya kuwa Mgombea
Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Tumeshiriki Uchaguzi tukiwa tukiwa kama Mayatima na Wakiwa, tumeweza kushinda
nafasi tulizo pata za kuwakilisha wananchi katika kata zetu katika mazingira
magumu bila ya uwepo na ushiriki wa Profesa Lipumba ambapombali na kudai kuwa
atabaki kuwa mwanachama wa kawaida na kuahidi kushiriki kampeni za majimbo hakuweza
kufanya hivyo hata katika Jimbo au Kata moja na si pekee kwa Dar es Salaam
hakushiriki kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015 katika maeneo yote
nchini,"alisema Omry.
Omry alisema kuwa wanapinga juhudi zote zinazofanywa na Profesa Lipumba
na wafuasi wake wote ambao wamekuwa na vitendo na mwenendo usio faa
wa kuharibu mali za Chama na kusababisha uvunjifu wa amani,kuharibu
taswira ya Chama mbele ya Jamii.
Kwa pamoja madiwani hao walisema wanatambua uwepo wa Kamati ya Taifa moja
inayoongozwa na Katibu Mkuu ,na Baraza Kuu la Uongozi mmoja ambalo wajumbe
wake wamepatikana kupitia Mkutano Mkuu wa Taifa wa Uchaguzi uliofanyika
Juni ,2014 Blue Pearl Hotel jijini Dar es Salaam.
Madiwani hao wote wameunga mkonom na kuheshimu hatua zilizochukuliwa na Baraza Kuu
hilo halali la CUF kuwa simamisha na Kuwavua uanachama Wanachama Wote ambao
wameshiriki kukiuka Kanuni na Maadili ya Chama chao kwa mujibu wa Katiba.
wamesma kuwa wanawapongeza viongozi wao wa Kitaifa wakiwemo Wajumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Taifa ,wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi, Wajumbe wa Baraza Kuu la
Taifa na Wabunge wao ambao wamekuwa mstari wa mbele kusimamia Chama katika kipindi
hiki cha mpito wa changamoto zinazowakabili na pongezi za pekee wamedai zimfikie
Jemedari wao Katibu Mkuu wa Chama Maalim Seif.
Comments