Waziri
Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi walio hudhuria
katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa
kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa
amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Na. Mwandushi Wetu
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji watakaokuja nchini kwa
kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na uchumi wenye
kukua kwa kasi.
Wazir Mkuu ameyasema hayo leo alipomuwakilisha Rais Dkt. John Pombe
Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan
alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Isamailia duniani
Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na
kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga
Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.
Waziri
Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni kwenye
maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu
mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani. Kushoto ni Rais wa Jumuiya
ya Shia Ismailia Amin Lakhani na (kulia) ni muwakilishi wa AKDN Resident
Amin Kurji, wakati alipomwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9,
2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ameupongeza mtandao wa taasisi za Aga
Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika kutoa kipaumbele cha
kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili
waweze kujikwamua kiuchumi.
“Nawahakikishia kwamba uwekezaji wenu
hapa nchini utakuwa na baraka kwa sababu nchi imetulia kisiasa na
uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa
madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini
fursa bado zipo.”
Waziri
Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akipokea maandano ya maadhimisho ya miaka 60
tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya
Shia Ismailia duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee,
Waziri Mkuu amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika sherehe hiyo,
Julai 9, 2017.
Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya
Madhehebu ya Shia Ismailia Tanzania, Bw. Amin Lakhani ameishukuru
Serikali kwa ushirikiano inaowapa na kwamba ameahidi kuendelea
kushirikiana nayo katika kuboresha sekta mbalimbali nchini.
Amesema mtandao wa maendeleo wa Aga Khan
unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za afya, elimu, kilimo na kunaendesha
miradi katika mabara ya Afrika na Asia kwa kuwapa fursa watu wenye
kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili kujikwamua kiuchumi.
Awali, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Bi.
Sophia Mjema aliipongeza taasisi hiyo kwa mpango wake wa upanuzi wa
hospitali na kuongeza vituo 35 vya afya kutoka 15 walivyonavyo.
Comments