KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AHIMIZA WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI NA TARATIBU KATIKA UTENDAJI KAZI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na washiriki wa mkutano wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni Mwenyekiti wa mafunzo (kulia) Bw. Paschal Mahinyika akiwatambulisha washiriki wa mafunzo ya kudhibiti viashiria hatarishi kabla ya kukaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinavyosimsmiwa na Wizara wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa uendeshaji wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Watendaji kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kutoka kulia ni Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu Bibi Deodata Makani , katikati ni Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi Bibi Martha chuma na kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bibi Lightness Mchome wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) katika ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu kwa kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Deodata Makani akitoa somo juu ya masuala ya kuzingatia kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni mwenyekiti wa mafunzo Bw. Paschal Mahinyika(kulia) wakati wa mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo vya maendeleo ya Jamii yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwasilisha mada kuhusu uaandaaji mzuri wa Bajeti kwa Wakuu wa Vyuo vua Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo hao yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati waliokaa)akiwa akiwa na wakufunzi wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakati wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi mahala pa kazi yaliyofanyikakatika Ukumbi wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo leo 31.7.2017. Picha na Erasto Ching’oro WAMJW
Na Erasto Ching’oro WAMJW
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kazi katika kuendesha vyuo wanavyovisimamia.
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu udhibiti wa viashiria hatarishi vya utendaji na utawala ikiwa ni pamoja na kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha katika utendaji wao wakazi wa kila siku ili kuepuka hoja za ukaguzi wa fedha.
Amesisitiza kuwa wakuu wa vyuo ni watumishi wa Umma na wanapaswa kuzingatia weledi mahala pa kazi kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zote za utumishi wa Umma katika kutimiza majukumu yao.
“Niwatake Wakuu wa Vyuo mliopo hapa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika kundesha vyuo mnavyoviongoza tuondokane na dosari katika suala la udhibiti wa Fedha katika matumizi” alisema Bibi Sihaba.
Aidha, Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga, amesema kuwa mara baada ya mafunzo haya maalum, Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini vitaweza kufuta hoja zote za ukaguzi mahala pa kazi kutokana na kufanya kazi kwa kufuata maadili, maarifa na miongozo na weledi unaotakiwa katika uendeshaji wa vyuo.
Aidha Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wakuu wa vyuo kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu yao mahala pa kazi, kuimarisha mawasiliano katika uwajibikaji wa pamoja kwa kuimarisha mifumo ya utendaji kazi katika vyuo vya maendeleo ya jamii.
Mafunzo haya yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na kushirikisha vyuo vya Buhare, Uyole, Rungemba, Ruaha, Mabughai, Monduli na Mlale.Source http://www.mtaakwamtaa.co.tz
Comments