CHAMA cha kutetea Abiria nchini (CHAKUA) kimeeleza kusua sua kwa mamlaka
husika katika sekta ya usafirishaji wa abiria .
Chakua kimetaja changamoto zinazo wakabiri kutokana na kutosikilizwa kilio
chao cha muda mrefu dhidi ya ukiukwaji wa makusudi wa taratibu za utoaji
wa huduma bora za usafirishaji kwenye Mabasi,Feri na Treni
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Chama
hicho Taifa Hassan Mchajama alisema kuwa wamekuwa wakipambana juu ya jitiada
za kuondoa changamoto alizozitaja na kuwa mstari wa mbele kuelimisha Umma(abiria),
na kuzungumza na mamlakahusika nje na ndani.
Alisema wamekuwa wakieelezea juu ya suala zima la urasimu mkubwa katika ukataji
na ununuzi tiketi za basi ambapo mfumo uliopo unamlazimisha abiria kupitia
kwa wapigadebe na mawakala ambao kazi yao kubwa imekuwa ni kulangua tiketi,"
alisema Mchajama.
"Hali nyingine inayojitokeza ni kusababisha upotevu wa mizigo utapeli na kutoa
taarifa za uongo kwa abiria ambapo katika mazingira kama hayo sisi kama CHAKUA
kama watetezi wa haki za abiria hatuwezi kuvumilia kunyamaza wakati sehemu
kubwa ya abiria wakizidi kutapeliwa,"alisema Mchajama.
Mchajama alisema kuwa hali ya wapiga debe imekuwa ikikosesha uhuru abiria
kuchagua huduma bora wanayotaka ndio maana wanaendelea kuikumbusha serikali
na mamlaka husika kuchukua hatua stahiki ili kuondoa kabisa mfano huo kiza
mani kandamizi.
Alisema hivi karibuni serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzani (TRA) ilitoa
matumaini ya kuanza kwa mfumo wa ukataji wa tiketi kwa njia ya kielektroniki
ambapo CHAKUA walifurahia sana kuunga mkono jitihada hizo za serikali .
Aidha kiongozi huo alisema kuwa wao kama wadau muhimu katika sekta
ya usafirishaji walialikwa na TRA katika vikao vyao kujadili namna bora
ya kutekelezauanzishwaji wa mfumo huo ambapo katika kikao cha Kamati Maalum
ya Kkufanikisha Uanzishwaji wa Mfumo Mpya wa Kielektironiki unaowahusisha TRA,
TABOA,SUMATRA,cHAKUA,JESHI LA POLISI cha Mei 30 mwaka huu waliweza
kupitisha na kukubaliana juu ya mfumo huo.
Pia makubaliano hayo walikubaliana waanze rasmi ambapo watoa huduma walitakiwa
kuanza kujiandaa kwa kuingiza taarifa kwenye mfumo wa E-Ticketing uliounganishwa
na mfumo wa TRA wa EFD.

Comments