Seif akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu mipango ya Ujenzi
wa Chuo Kikuu cha Kiislam kinachojengwa katika eneo hilo la kinondoni.
BODI ya wadhamini ya Masjid Ridhwaa (RTMR) Mkwajuni Kinondoni
jijini Dar es Salaam kuanza ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kiislam nchini
kitakachowezesha wahitimu kujiajili na kuajiliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini Alhaj Suleiman Seif Nassor alisema ujenzi huo unakadiriwa kuwa
wa ghorafa tano ambao utagharimu shilingi bilioni 2 za kitanzania
pia alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuri kwa kazi nzuri katika kipindi kisichozidi miaka 2.
Alhaj Seif alisema Chuo hicho kinatarajia kutoa wahitimu wenye sifa ya
kujiajiri na kutoa ajira za kwanza baada ya kuhitimu masomo yao hususani
wanafunzi wa fani ya uandishi wa habari.
"Tumefurahishwa sana kwa Rais Magufuli kwa namna alivyofanikiwa kuinyoosha
nchi Umma,kuwaokoa vijana wengi waliojiingiza katika biashara ya madawa ya
kulevya ,'alisema Alhaj Seif.
Alisema kupitia taasisi ya (MUTA)imejipanga kuajili walimu wasiopungua 42, na
madhumuni yake ni kujenga misikiti,vituo vya elimu,vituo vya afya na kufanya
miradi ya uchumi kwa kuzingatia misingi ya kiislam pamoja na kufanya
mambo yote ya maendeleo.
Aidha azma kubwa ya MUTA ni kuendeleza vijana kitaaluma na kisayansi kwa
kuzingatia sera ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga Tanzania ya viwanda
vya kati.
Pia Alhaj Seif alisema wameitaka serikali ya Rais Magufuli kubaini na kubadili
muundo wa shahada uliopo sasa kwa kuandaa watafuta ajira serikalini na kwenye
makampuni binafsi badala yake kuandaa masomo yatakayo waandaa kujiajili tangu
wakiwa katika mwaka wa pili wa masomo ya kidigitali.
Tumepania kutoa mchango kwa kuitikia wito wa Rais Magufuli wa kuanzisha
viwanda vya kati kwa kuweka wasomi wenye mwelekeo wa kidigitali kwa mafunzo
na vitendo zaidi ili kuondoa ugonjwa sugu kwa wahitimu kutafuta kazi.
Comments