Kinachofanywa na Ac Milan sokoni kwa sasa hakika ni fujo,
inasemekana klabu hiyo ya nchini Italia sasa imehamishia majeshi yake
kwa Alvaro Morata na wako tayari kuwapa Real Madrid £70 ili kumnunua.
Golikipa wa zamani wa klabu ya Manchester City Joe Hart anakaribia
kukamilisha uhamisho wake kwenda West Ham na ripoti zinasema hii leo
Hart atafanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na wagonga nyundo hao.
Katika kuonesha kwamba siku zake Chelsea zinakaribia kuisha, Diego
Costa ameonekana akila raha kijijini kwao Brazil huku akiwa amevaa jezi
ya timu yake ya zamani ya Atletico Madrid.
Manchester United wanakaribia kumsaini winga wa klabu ya Inter Millan
Ivan Perisic ambapo inasemekana usajili wa winga huyo unaweza
kukamilika mwishoni mwa wiki hii.
Baada ya Ross Barkley kutoswa katika safari ya Everton kuja Bongo
sasa kiungo huyo yuko mbioni kuhamia Tottenham ambapo taarifa zinadai
kwamba klabu ya Tottenham iko tayari kutuma ofa nono ili kumpata.
Kocha wa Arsenal anaonekana amedhamiria kufanya makubwa ambapo sasa
yuko mbioni kutuma ofa mbili kumnunua mlinzi Virgil Van Dijik na
mshambuliaji wa Celtic Moussa Dembele.
Ukiachana na usajili wa Dijik na Dembele inasemekana Arsenal
wanakaribia kumnunua mlinzi wa Monaco Thomas Lemar ambaye thamani yake
inatajwa kuwa £45m.
Comments