Dar es Salaam.Chuo Kikuu Cha Sebastian Kolowa cha Mjini Lushoto Mkoani Tanga
kimejidhatiti katika kutoa elimu bora kwa makundi yote katika fani mbali mbali
zitolewazo na Chuo hicho.
Akizungumza na Mwandishi wa gazeti hili katika maadhimisho ya wiki ya vyuo vikuu
yaliyo kuwa yakiadhimishwa katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Dakt Anneth Munga Makamu Mkuu wa Chuo hicho amesema katika kuadhimisha miaka kumi,yakuanzishwa kwa chuo hicho,Chuo kimedhamiria kutoa elimu bora zaidi kwakuimarisha miundo mbinu yakusomea
chuon hapo.
“Ni miaka kumi tokea kuanzishwa kwa Chuo hiki,shabaha yetu ikiwa ni kutoa elimu bora ambayo
inaendana na miundo mbinu bora ya kusomea hususani kwa wanafunzi wanao soma kozi ya watu wenye mahitaji maalumu,"alisema Dakt Anneth.
Dakt Anneth lisem kuw Sanjari na hilo chuo hicho ni chuo pekee nchini kinachotoa taaaluma kwa
watu wenye mahitaji maalumu hususani ,kwa watu wenye mahitaji maaalumu kusomea taaluma mbali mbali zitolewazo chuoni hapo pamoja na wao wao kusoma taaluma hiyo.
Ikilinganishwa na Vyuo vingine ambavyo hutoa elimu ya watu wenye mahitaji maalumu ambapo hutoa taaluma hiyo kwa watu ambao wanakwenda kuwahudumia watu wenye mahitaji maalumu.
Miongoni mwa uboreshaji miundombinu yakusomea ambayo imeboreshwa na ya kisasa zaidi ni moja ya jengo lakisasa lijulikanalo kama ghorofa la Benjamini Mkapa ambalo linavifaa vya kisasa vya kufundishia na rafiki kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Maadhimisho hayo yatafikia kilele chake tarehe 28 Oktoba 2017,ambapo kwa sasa chuo hicho kinaadhimisha maadhimishohayo kila mwisho wa mwezi ikihuisha shughuli mbali mbali za kimazingira na kimaendeleo chuoni hapo na katika vituo vyake.
Comments