- Folk Development College ( FDC)
Tanzania viko 55. Mwalimu Julius Nyerere
alikuwa muasisi wa vyuo hivi baada ya kufanya ziara nchini Sweden na
kutembelea moja ya vyuo hivyo.
Ni Nordic idea ambayo inafaa katika
mazingira yetu pia. Falsafa kuu ya vyuo hivi ni kumpa nafasi mwananchi
kujifunza katika mazingira yake na kwa kuanzia kutokana na uzoefu wake.
Ni hata kama mwananchi huyu ameishia
darasa la saba, kukatishwa masomo yake kwa sababu moja au nyingine, au
hakubahatika kabisa kwenda shule.
Na tunaposema tunataka kuingia kwenye
uchumi wa viwanda, basi, tunawahitaji pia mafundi mchundo. Ni vyuo kama
hivi vinavyoweza kuzalisha vijana kama hao kwa wingi. Ni bahati mbaya
kuwa umuhimu wa vyuo ulikuwa bado haujafahamika kwa watunga sera wetu
wengi. Serikali ya Awamu ya Tano imeonyesha kuvitambua vyuo hivi na
jukumu lake katika jamii.
Itakumbukwa, Mei , 2016, Rais Barack
Obama aliwaalika mawaziri wa Elimu kutoka nchi za Nordic na katika
hotuba yake alisifu wazo la Folk High Schools kwa kusema...
"And many of our Nordic friends are
familiar with the great Danish pastor and philosopher Grundtvig. And
among other causes, he championed the idea of the folk school —
education that was not just made available to the elite but for the
many; training that prepared a person for active citizenship that
improves society. Over time, the folk school movement spread, including
here to the United States. And one of those schools was in the state of
Tennessee — it was called the Highlander Folk School."- Barack Obama
Comments