Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2017

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AHIMIZA WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI NA TARATIBU KATIKA UTENDAJI KAZI

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.   Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na washiriki wa mkutano wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.  Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni Mwenyekiti wa mafunzo (kulia) Bw. Paschal Mahinyika akiwatambulisha washiriki wa mafunzo ya kudhibiti viashiria hatarishi kabla ya kukaribisha...

Dakt Anneth Munga: Sekomu chuo pekee nchini kinachotoa taaaluma kwa watu wenye mahitaji maalumu

Dar es Salaam.Chuo Kikuu Cha Sebastian Kolowa cha Mjini Lushoto Mkoani Tanga  kimejidhatiti katika kutoa elimu bora kwa makundi yote katika fani mbali mbali  zitolewazo na Chuo hicho. Akizungumza na Mwandishi wa gazeti hili katika maadhimisho ya wiki ya vyuo vikuu yaliyo kuwa yakiadhimishwa katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Dakt Anneth Munga Makamu Mkuu wa Chuo hicho amesema katika kuadhimisha miaka kumi,yakuanzishwa kwa chuo hicho,Chuo kimedhamiria kutoa elimu bora zaidi kwakuimarisha miundo mbinu yakusomea  chuon hapo.  “Ni miaka kumi tokea kuanzishwa kwa Chuo hiki,shabaha yetu ikiwa ni kutoa elimu bora ambayo  inaendana na miundo mbinu bora ya kusomea hususani kwa wanafunzi wanao soma kozi ya watu wenye mahitaji maalumu,"alisema Dakt Anneth. Dakt Anneth lisem kuw Sanjari na hilo chuo hicho ni chuo pekee nchini kinachotoa taaaluma kwa  watu wenye mahitaji maalumu  hususani ,kwa watu wenye ...

CHAKUA:Wajajuu kuhusu kusua sua kwa mamlaka husika katika sekta ya usafirishaji

CHAMA cha kutetea Abiria nchini (CHAKUA) kimeeleza kusua sua kwa mamlaka husika katika sekta ya usafirishaji wa abiria . Chakua kimetaja changamoto zinazo wakabiri kutokana na kutosikilizwa kilio chao cha muda mrefu dhidi ya ukiukwaji wa makusudi wa taratibu  za utoaji wa huduma bora za usafirishaji kwenye Mabasi,Feri na Treni Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Hassan Mchajama alisema kuwa wamekuwa wakipambana juu ya jitiada za kuondoa changamoto alizozitaja na kuwa mstari wa mbele kuelimisha Umma(abiria), na kuzungumza na mamlakahusika nje na ndani. Alisema wamekuwa wakieelezea juu ya suala zima la urasimu mkubwa katika ukataji na ununuzi  tiketi za basi ambapo mfumo uliopo unamlazimisha abiria kupitia kwa wapigadebe na mawakala ambao kazi yao kubwa imekuwa ni kulangua tiketi," alisema Mchajama. "Hali nyingine inayojitokeza ni kusababisha upotevu wa mizigo utapeli na kutoa taarifa za uongo kwa abiria ambapo katika mazingira k...

TFF YAMTOA KIFUNGONI HAJI MANARA

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefuta adhabu dhidi ya wanafamilia wanne waliofungiwa kushiriki masuala la soka kwa mwaka mmoja.   Wanafamilia hao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa, James Mwakwinya; Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Blassy Kiondo; Kaimu Katibu wake, Ayoub Nyaulingo pamoja na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara. Haji Manara alitiwa hatiani Aprili 23, mwaka huu kwa makosa ya lugha chafu na za chuki kwa viongozi wa TFF na kupotosha umma dhidi ya kadi njano ya mchezaji Mohammed Fakhi wa Kagera Sugar ambako alifungiwa kushiriki masuala ya mpira kwa mwaka mmoja na faini ya Sh milioni tisa. Viongozi wa RUREFA walifungiwa kwa mwaka mmoja na faini ya Sh. milioni mbili kwa kila mmoja kwa makosa ya kukiuka maagizo ya viongozi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyotaka wasitishe mchakato wa uchaguzi mkoa kwa kuwa kulikuwa na rufaa iliyokat...

TCU: Udahili Vyuo Vikuu Kuanza Julai 22

Na: Lilian Lundo - MAELEZO. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU) umeutangazia Umma kuwa kuanzia Julai 22 mwaka huu vyuo vyote vya elimu ya juu hapa nchini vitaanza kupokea maombi ya udahili kwa mwaka wa masomo  2017/2018. Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Eleuther Mwageni ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya kuanza rasmi udahili kwa mwaka 2017/2018. Prof. Mwageni amesema kuwa waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao  kwenye vyuo husika na siyo tena TCU kama ilivyokuwa kwa mwaka jana na miaka mingine ya nyuma. Aidha amesema kuwa waombaji wahakikishe wanaomba programu za masomo ambazo zimeidhinishwa na kutambuliwa na TCU na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). "Tunavikumbusha vyuo kutangaza programu ambazo zimeidhinishwa na kutambuliwa na TCU na NACTE, ikiwa chuo kitatangaza programu ambazo  hazitambuliki na Tume, basi chuo husika kitachukuliwa hatua," amesema P...

Mbunge wa Temeke ahukumiwa kwa kuendesha gari bila Bima na kutotii amri ya Polisi

Mbunge wa Temeke Mhe. Abdalah Mtolea jana alipandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Temeke akikabiliwa na mashataka mawili ikiwemo la kuendesha gari bila ya bima kinyume na sheria za nchi. Mbunge huyo kwa tiketi ya chama cha wanachi CUF, alisomewa mashtaka yake mbele ya hakimu mkazi Mhe. Eliarusia Nassatri mbale ya mwendesha mashtaka wa serikali Joseph Maugo ambaye aliiambia mahakama hiyo kuwa katika kosa la kwanza Mbunge huyo anadaiwa kuendesha gari ambalo halina bima Maelezo ya kosa hilo yanadai kuwa, Julai 19 mwaka huu katika barabara ya Kilwa eneo la Bendera tatu, mshtakiwa alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 672 BNV Toyota Mark 2 likiwa halina bima. Katika kosa la pili, mshatakiwa Mtolea anadaiwa kulitenda muda na eneo la kwanza alipotenda kosa la kwanza kwakushindwa kutekeleza agizo la ofisa Polisi mwenye namba F 818 Kopla Robati la kutakiwa kupeleka gari hilo katika kituo cha Polisi Kilwa Road lakini mshtakiwa ...

Msichana wa Ujerumani ''aliyejiunga na IS akamatwa Iraq'' Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpya

Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Mji wa Mosul nchini Iraq Viongozi wa mashtaka nchini Ujerumani wanachunguza iwapo msichana wa miaka 16 kutoka Ujerumani ni miongoni mwa kundi la washukiwa wa Islamic State waliokamatwa mjini Mosul. Aliripotiwa kupatikana na vikosi vya kijeshi katika handaki katika mji huo wa Iraq siku ya Alhamisi pamoja na raia wengine 19 wa kigeni. Maafisa wanajaribu kuthibitisha iwapo ni msichana huyohuyo aliyepotea kutoka mji wa Ujerumani wa Lulsnitz mwaka uliopita. Serikai ya Iraq imetangaza ushindi dhidi ya IS mjini Mosul ,ijapokuwa vita vinaendelea katika maeneo mengine ya mji huo wa zamani. Vita hivyo ambavyo vimechukua miaka tisa viliyawacha maeneo makubwa yakiwa yameharibiwa na kuwaua maelefu ya raia huku takriban watu 920,000 wakiwachwa bila makao. Picha za msichana huyo aliyekamatwa na wanajeshi wa Iraq zilichapishwa na vyombo vya habari vya eneo hilo. Chombo cha habari cha Ujerumani DPA kiliripoti kuwa kundi hilo la wageni lilikuw...

Wanajeshi 800 wastaafishwa nchini Rwanda

Haki miliki ya picha AFP Image caption Wanajeshi wa Rwanda hulinda amani katika nchi kadha Afrika Askari jeshi zaidi ya 800 wakiwemo baadhi ya maafisa wakuu katika jeshi la Rwanda wamestaafishwa. Miongoni mwa waliostaafishwa ni majenerali wawili waliowahi kuongoza idara za upelelezi za nchi hiyo, Jenerali Karenzi Karake na Jenerali Jack Nziza. Mwaka uliopita majenerali hao walibadilishiwa nyadhifa walizokuwa nazo jeshini, hatua ambayo kwa baadhi waliifasiri kuwa kama kushushwa ngazi. Kulingana na wizara ya ulinzi ya Rwanda baadhi ya waliostaafishwa wamekamilisha mikataba yao jeshini na wengine ni kutokana na sababu za ugonjwa. Mwandishi wa BBC aliyepo Kigali Yves Bucyana anasema kwa jumla maafisa waliostaafishwa ni 817. Luteni jenerali Karenzi Karake kwa muda mrefu aliongoza idara ya upelelezi ya Rwanda na nje ya mipaka ya nchi hii akawa naibu kamanda wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan. Naye Brigedia jenerali Jacques N...

Taarifa iliyotolewa na Serikali baada ya kauli za jana za Tundu Lissu

Serikali imemshauri Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu kutekeleza wajibu wake kwa kusimamia weledi akiwa kama Wakili wa Mahakama Kuu badala ya kufanya Propaganda kwa kutumia lugha ya kejeli, kuudhi na uchochezi kuituhumnu Serikali kuwa inabana demokrasia. Alieyasema hayo leo ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi katika taarifa kwa Umma aliyoitoa juu ya ufafanuzi kuhusu propaganda na upotoshaji wa Mbunge huyo. “Vyombo mbalimbali vya habari leo vimemnukuu Mbunge wa Singida Mashariki Ndugu Tundu Lissu ambapo pamoja na mambo mengine, huku wakati fulani akitumia lugha za kuudhi, uchochezi na kejeli, ameituhumu Serikali kuwa inabana demokrasia nchini,” imefafanua taarifa hiyo. Taarifa hiyo imesema kuwa madai kwamba Serikali inakandamiza demokrasia ni propaganda tu za kisiasa, kutokana na Lissu kuone...

Banda huyoooo Ifahamu zaidi Baroka FC

  Na Salym Juma, Arusha Nikinukuu kauli ya Abdi Banda katika maandishi kwamba, wachezaji wajitume na wanatakiwa kuwa makini na nafasi, hasa zinapotokea nafasi za kutoka kwenda kucheza nje ya nchi na wasiangalie nyuma. Kauli ya Beki huyu wa zamani wa Simba inawagusa Wachezaji ambao wanaamini Simba na Yanga ndio sehemu pekee ya mafanikio ambayo wanapaswa kufika. Ukweli ni kwamba hata hao akina Samatta na Ulimwengu walifika hapo walipo baada ya kuondoka Tanzania na kwenda kujaribu bahati zao nje. Kufanya vizuri kwa Abdi Banda msimu uliopita kumemfanya mchezaji huyu kupata nafasi ya kusajiliwa na timu iliyoshiriki ligi kuu ya South Afrika msimu uliomalizika. Banda ambaye tayari alishasaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo wakati akiwa kwenye michuano ya COSAFA Cup 2017 iliyofanyika South Afrika anakwenda kucheza kwenye ardhi ya Mandela na kama akikitumia vyema kipaji chake huenda akapata shavu kwenye vilabu vikubwa vya South Afrika. Banda ni a...

Hapa Wenger hataki utani !!

Kinachofanywa na Ac Milan sokoni kwa sasa hakika ni fujo, inasemekana klabu hiyo ya nchini Italia sasa imehamishia majeshi yake kwa Alvaro Morata na wako tayari kuwapa Real Madrid £70 ili kumnunua. Golikipa wa zamani wa klabu ya Manchester City Joe Hart anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda West Ham na ripoti zinasema hii leo Hart atafanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na wagonga nyundo hao. Katika kuonesha kwamba siku zake Chelsea zinakaribia kuisha, Diego Costa ameonekana akila raha kijijini kwao Brazil huku akiwa amevaa jezi ya timu yake ya zamani ya Atletico Madrid. Manchester United wanakaribia kumsaini winga wa klabu ya Inter Millan Ivan Perisic ambapo inasemekana usajili wa winga huyo unaweza kukamilika mwishoni mwa wiki hii. Baada ya Ross Barkley kutoswa katika safari ya Everton kuja Bongo sasa kiungo huyo yuko mbioni kuhamia Tottenham ambapo taarifa zinadai kwamba klabu ya Tottenham iko tayari kutuma ofa nono ili kumpata. Kocha wa Arsenal anaon...

Neymar sasa kufuatwa na PSG kwa nguvu zote

  Katika kuonesha jeuri ya pesa matajiri wa kiarabu wanaoimiliki klabu ya PSG wamepiga hodi katika klabu ya Barcelona tayari kwa ajili ya kuvunja rekodi ya dunia kumtwaa mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar. Taarifa zinasema kiasi cha zaidi ya £200m ambayo ni mara mbili na zaidi ya pesa zilizotumika kumnunua Paul Pogba ambaye kwa sasa ndio anashikilia rekodi ya usajili ya dunia kwa sasa. Ripoti zinasema klabu ya PSG inataka kutumia mwanya wa Neymar kukosa uhuru wa kucheza free mbele ya Messi hivyo wanataka kutuma ofa ya karibia £222m ambayo ni wazi itawashawishi Barcelona kumuuza. Katika dili hiyo Neymar atakula £30m kila mwaka na uwepo wa Dani Alves katika kikosi cha PSG unaweza kuwa ushawishi mkubwa kwa Neymar na PSG wanaweza kumtumia mlinzi huyo kumshawishi Neymar. Habari zinasema Neymar hana furaha na Barcelona kwani ni ngumu kuchukua tuzo ya Ballon D’Or ukicheza mbele ya Suarez na Messi ambapo washambuliaji hao wanaminya uhuru wa Neymar aki...

Stars kuanza safari ya Rwanda

Kikosi cha timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda kesho Jumatano mchana kikitokea Mwanza, Tanzania. Taifa Stars iliyokuwa jijini Mwanza kwa kambi kabla ya kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Rwanda Jumamosi iliyopita, itapitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere kwenda Rwanda. Stars itaondoka Mwanza kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania majira ya saa nne asubuhi na kuwasili Dar es Salaam majira ya saa sita mchana kabla ya kuunganisha ndege ya Rwanda majira ya saa nane alasiri kwenda Kigali, Rwanda. Inakwenda Kigali kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Rwanda maarufu kama Amavubi kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN 2018). Fainali za CHAN mwakani zitafanyika nchini Kenya. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa CCM Kiru...

Laurence Mabawa afunguka

MDAU amejitokeza kuiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kuwachukulia hatua kali za kisheria wote wanaotumia mitandao ya kijamii kwa nia mbaya . Mbali na suala hilo kuwa limezungumzwa mara kwa mara BW.Laurence Mabawa amewaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam kuwa watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari wakidai kuwa watu wanaojitokeza kumpongeza Mh.Rais John Pombe Magufuli kuwa wanajipendekeza jambo ambalo si kweli. Alisema kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 18 inatoa haki kwa kila mtanzania kutoa maoni yake bila kuvunja katiba. "Kwa hiyo kitendo cha Raia yeyote kushambulia kwa maneno makali na yakuhudhi kwa uamuzi wake wa kutoa maoni kwa kile anachokiona hakikubariki hata kidogo,"alisema Mabawa. Alisema kama jinsi watanzania na wasio watanzania tunavyo tambua kazi kubwa na nzuri ya kutetea na kupigania rasilimali za taifa inayofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ch...

Alhaj Suleiman Seif:Masjid Ridhwaa kuanza ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kiislam nchini

 Pichani Mwenyekiti Bodi ya wadhamini ya Masjid Ridhwan Alhaj Suleiman Seif akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu mipango ya Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kinachojengwa katika eneo hilo la kinondoni. BODI ya wadhamini ya Masjid Ridhwaa (RTMR) Mkwajuni Kinondoni jijini Dar es Salaam kuanza ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kiislam nchini kitakachowezesha wahitimu kujiajili na kuajiliwa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Alhaj Suleiman Seif Nassor alisema ujenzi huo unakadiriwa kuwa wa ghorafa tano ambao utagharimu shilingi bilioni 2 za kitanzania pia alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuri kwa kazi nzuri katika kipindi kisichozidi miaka 2. Alhaj  Seif alisema  Chuo hicho kinatarajia kutoa wahitimu wenye sifa ya kujiajiri na kutoa ajira za kwanza baada ya kuhitimu masomo yao hususani wanafunzi wa fani ya uandishi wa habari. "Tumefurahishwa sana kwa Rais Magufuli kwa namna alivyo...

Mh.Samia Suluhu:amezinduahuduma za kifedha za kampuni ya simu ya Tanzania (TTCL PESA))

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan jana amezinduahuduma za kifedha za kampuni ya simu ya Tanzania (TTCL Pesa). Akizungumza katika uzinduzi huo Dar es Salaam kwenye Makao Makuu ya Kamupuni hiyo alisema uzinduzi huo uwemwendelezo wa jitihada za kulejea katika nafasi ya kuwa suluhisho la kweli la utoaji Hhuduma za Mawasiliano hapa nchini. Alisema kuzinduliwa kwa huduma hiyo iwe uthibitisho mwingine yakwamba TTCL  inatekeleza maagizo ya serikali ya awamu ya tano nchini ambapo Rais wetu DKT,John Pombe Magufuli alielekeza kuwa mashirika yote ya Umma yajiendeshe kwa faida. "Mashirika ya Umma yajiendeshe kwa faida, yatoe gawio serikalini, yawahudumie wananchi kwa kiwango cha juu cha ubora na kwa gharama nafuu,"alisema Mh.Samia. Samia alisema anawapa hongera TTCL kwa kutekeleza maagizo hayo kwa vitendo na kuchukua fursa ya kuwapongeza kwa ushindi walioupata hivi karibuni kwa kushika nafasi ya kwanza katika ...

Venus Williams amtupa nje Johanna Konta michuano ya Wimbledon

Matumaini ya Muingereza Johanna Konta kufika fainali za Wimbledon yamefutiliwa mbali baada ya kuchapwa na Venus Williams wa Marekani katika hatua ya nusu fainali. Venus mwenye miaka 37 alicheza kwa umakini mkubwa zaidi na kushinda kwa seti 6-4 6-2. Konta anayeshikilia nafasi ya sita kwa ubora duniani, alitegemea kufika fainali hizo na kuwa wa kwanza kufanya hivyo kwa Uingereza tokea mwaka 1977. Image caption Konta anasema alitegemea upinzani mkali kutoka kwa Venus Matumaini pekee kwa Konta ni kuingia ndani ya tano ...

Wayne Rooney aiongoza Everton kuilaza Gor Mahia Tanzania

Wayne Rooney ameiongoza klabu yake mpya Everton kuishinda klabu ya Kenya ya Gor kwa kufunga bao zuri katika mechi ya kirafiki iliodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa. Mchezaji huyo alirudi katika klabu yake ya utotoni baada ya kuichezea Manchester united kwa takriban miaka 13. Rooney aliiweka kifua mbele Everton kunako dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza ambacho Gor Mahia ilionekana kucheza vizuri kuwashinda wageni hao. Hatahivyo Gor Mahia haikusubiri kwani baada ya mpira kuanzishwa katikati walipata kona iliopigwa na George Odhiambo ambapo ilimpata JacquesTuyisenge katika eneo zuri na hivyobasi kusawazisha kupitia kichwa kikali ambacho kipa wa Everton alishindwa kuokoa. Kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza timu hizo zilikuwa na sare ya 1-1. Timu zote mbili zilifanya mabadiliko huku Rooney akitolewa baada ya kipindi cha kwanza Bao la Rooney lilirudisha kumbukumbu za bao lake dhidi ya Arsenal akiichezea Everton. Katika kipindi cha pili Ever...

Acacia yakubali kuilipa TanzaniaAcacia yakubali kuilipa Tanzania

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imekubali kuilipa serikali ya Tanzania nyongeza ya mrabaa wa kati ya asilimia 4 mpaka 6 kama ilivyoainishwa kwenye muswada wa sheria mpya ya madini nchini humo. Serikali ya Tanzania na kampuni ya Acacia ziliingia katika mgogoro mapema mwezi tatu mwaka huu kutokana na kuzuiliwa kwa makontena 256 ya Mchanga wa dhahabu (makinikia) kwenye bandari ya dar es salaam baada ya kubainika kuwa Acacia haitoi taarifa sahihi ya kiwango cha madini kilichopo katika mchanga huo hivyo kulipa tozo zisizo sahihi kwa karibu miongo miwili jambo ambalo linapingwa vikali na kampuni hiyo.Chanzo BBC.

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YAILILIA AMREF

Na Carlos Nichombe Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo ameliombaShirika la Utafiti wa Tiba na Afya barani Afrika (AMREF) kujenga ofisi Visiwani Zanzibar ili kuisaidia Serikali katika kupambana na tatizo la vifo vya mama na mtoto. Kombo aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wadau mbambali wa Masuala ya Afya waliojitokeza katika maadhimisho ya miaka 60 ya uanzishwaji wa Shirika la AMREF. Alisema AMREF wamekuwa na mchango mkubwa nchini Tanzania hususani katika ukomeshaji vitendo vya ukeketaji kwa wanawake katika maeneo mbalimbali hivyo kuwaomba waigeukie na Zanzibar kwa ajili ya utatuzi wa masuala mbalimbali yanayowasumbua. Alieleza kuwa jukumu la kutokomeza vifo vya mama na mtoto ni la jamii yote hivyo kama shirika hilo litajenga ofisi zao visiwani Zanzibar litaongeza nguvu kwa Serikali ambayo  imekuwa ikitafuta wadau mbalimbali katika kutatua matatizo hayo. “Najua mmefanya juhudi nyingi ambazo ki...