Na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dodoma
Baadhi ya
Wabunge wanaotoka Kanda ya Ziwa wameomba Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na
Mawasiliano kujenga Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kiwango cha Kimataifa
ili kuimarisha sekta ya Utalii na usafiri wa anga katika kanda ya Ziwa.
Walisema
kuwa hatua itasaidia watalii wanaokuja nchini kushuka moja kwa moja
mkoani Mwanza na kisha kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na
maeneo mengine ya vivutio vya hapa nchini bila kupitia nchi jirani.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Wabunge Dkt.Raphael Chegeni na Mhe. Ezekeil
Maige wakati wakichangia hotuba kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara
ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka ujao wa fedha.
Mhe.
Dkt.Chegeni alisema kuwa Uwanja wa Ndege wa Mwanza ni muhimu ukajengwa
kwa viwango vya Kimataifa ili uweze kuruhusu ndege mbalimbali kubwa na
ndogo kuweza kutua bila tatizo.
Alisema
kuwa hatua hiyo itasaidia kuunganisha Mkoa wa Mwanza na nchi jirani za
Rwanda, Uganda na Burundi na hivyo kuruhusu ndege nyingi kutoka Nchi
hizo kutua bila kwenda katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere .
Mhe. Dkt.
Chegeni aliongeza kuwa uwanja huo endapo utajengwa kwa kiwango cha
Kimataifa utasaidia kuwa kiungo muhimu kwa mikoa 10 ya kanda ya ziwanana
kati.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Maige alisema kuwa ujenzi wa Uwanja wa
Ndege wa Mwanza sio tu utasaidia kuunganisha mkoa huo na mikoa mingine
bali utasaidia kuchochea uchumi wa eneo la Kanda ya Ziwa na Tanzania
kwa ujumla kwani watalii na wasafiri wengine watakuwa na fursa ya
kuingia Mwanza bila kupitia nchi jirani.
Aliongeza
kuwa endapo zoezi hilo litafanyika kwa kiwango cha kimataifa litatoa
fursa kwa ndege nyingi za ukumbwa tofauti tofauti kutua katika Uwanja
huo na hivyo kupunguzia wananchi ughali wa bei unaotozwa na baadhi ya
Kampuni za Ndege ambazo zinatoa huduma za usafiri mkoani humo.Iinatoka http://www.mjengwablog.com/
Comments