Wakati timu ya Simba ikiendelea kufanya vibaya beki wa kulia wa Simba SC, Hassan Ramadhani Kessy (katikati) akitia dole gumba kwenye fomu za mkataba wa kujiunga na Yanga
Kuna
msemo wa Kiswahili unasema ‘ukisusa wenzio wala’, msemo huu umetimia
baada ya beki wa kulia wa kikosi cha Simba SC Hassan Kessy kutia
dolegumba kwenye fomu za usajili za Yanga na kujiunga na mabingwa hao wa
mitaa ya Twiga na Jangwani.
Kessy ametia saini juzi mkata wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka miwili kuanzia mwezi ujao (June, 2016).
Awali Kessy alikuwa akiitumikia klabu ya Simba kabla ya kufungiwa
mechi tano na wekundu hao wa Msimbazi kwa madai ya kuigharimu timu
kutokana na kitendo cha kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi
dhidi ya Toto Africans mchezo uliomalizika kwa Simba kupoteza kwa bao
1-0.
Licha ya Simba kumfungia Kessy, tayari beki huyo mwenye uwezo mkubwa
wa kukaba ns kupandisha mashambulizi mkata wake wa na Simba unamalizika
mwisho wa msimu huu na klabu hiyo haikuonesha nia ya kuhitaji huduma ya
nyota huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar.
Comments