Miss Dar city center Talent ilivyofana jana
HATIMAYE shindano la
kumtafuta Miss Dar City Centre Talent limefanyika usiku wa alhamisi katika Ukumbi wa
Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar.
Katika kinyang’anyiro hicho, kilichoshirikisha warembo kibao hatimaye
mrimbwende Sporah Luhende aliibuka mshindi wa kipaji baada ya kuimba
Wimbo wa Mahaba Niue wa msanii Maua Sama.
Kilele cha shindano hilo la warembo linatarajiwa kuwa Mei 21, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip City Centre.
Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers kupitia
Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa kupitia Magazeti ya
Championi, Ijumaa, Risasi, Amani, Uwazi ambapo droo ya ndogo ya bahati
nasibu hiyo itachezeshwa Mei, 18 na droo kubwa yenye ushindi wa nyumba
itachezeshwa mwezi ujao.
Comments