Rapa 50 Cent ameomba radhi familia ya kijana mlemavu wa akili
kwa kupost video ya kijana huyu akiwa kazini na kusema ametumia kilevi
flani huku akifanya kazi kwenye uwanja wa ndege nchini Marekani.
50 Cent alipondwa vikali na mashabiki wake kwa kitendo hicho
alichomfanyia kijana huyu huku familia yake ikitaka awaombe radhi uso
kwa uso na kulipa faini ya dola milioni moja.
50 Cent ameomba radhi kwa kuandika barua kumuomba msamaha kijana huyo aitwaye Andrew Farrell.
Na sasa familia yake imemtaka 50 cent alipe dola 100,000 kwa taasisi
ya Autism Speaks, Mchango huo ni mdogo zaidi ukilinganisha na dola
milioni 1 ambazo baba wa kambo wa Andrew alitaka walipwe.
Comments