Farid
alitafutiwa timu hiyo na wakala wake ambaye hapo awali Farid ilikuwa
apelekwe moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga,
kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao kwa majaribio, lakini wakala
wake akashauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania
ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka.
Baada ya majaribio na Klabu ya Tenerife, Farid alifanya vizuri na
Klabu hiyo ikakubali kiwango chake hivyo Farid anarejea nchini kusubiria
mazungumzo ya Klabu yake ya Azam fc na Tenerife ili kuweza kuitumikia
klabu hiyo.
Farid alikwenda Hispania Aptili 21 mwaka huu akitoka kuichezea klabu
yake, Azam FC katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la
Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance.
Comments