Mara nyingi tumekuwa tukisema tabia zako ulizonazo ndizo
zinazopelekea maisha yako yawe bora au mabovu. Ni jambo ambalo tumekuwa
tukikumbushana kwamba siku zote maisha ya binadamu yanaongozwa na tabia
alizonazo binadamu huyo. Kwa mantiki hiyo, ikiwa na maana kwamba kwa
kujijengea tabia za aina fulani kwenye maisha yako, ndivyo maisha yako
yataendelea kuwa hivyo kama tabia zako jinsi zilivyo.Tatizo
walilonalo wengi ambalo linakuwa linawasumbua sana ni kule kurudishwa
nyuma na tabia zao. Utakuta mtu anauwezo mzuri kabisa wa kutengeneza
pesa za kutosha lakini kila wakati anakuwa hana au anaishi maisha ya
kimaskini kwa sababu ya kujijengea tabia mbaya. Ili kufanikiwa unatakiwa
kutambua mapema tabia zinazo kurudisha nyuma kimafanikio. Je, unajua ni
tabia gani zinazokurudisha sana nyuma kwenye maisha yako?1. Kuamini maisha ni magumu.Siku
zote ukweli wa maisha uko hivi; ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe
chanya kwanza. Lakini kwa bahati mbaya wengi wetu hawako hivi. Ni watu
wa kuamini sana maisha hasi ikiwa pamoja na kuamini maisha ni magumu.
Mara nyingi wengi wetu tumelishwa imani ya kwamba maisha ni magumu sana
na kusahau tu kwamba maisha yanachangamoto ambazo zinatakiwa kutatuliwa
kila siku.Ukitaka kuelewa vizuri juu ya hiki
ninachosema, jaribu kumuuliza kila unayekutana naye ' Maisha vipi?' Au
mwambie 'maisha yanaendaje?'. Wengi kati yao watakwambia maisha ni
magumu sana. Kwa kuwa na Imani hii maisha ni magumu inawarudisha wengi
nyuma kimafanikio kwa sababu akili zao zote zinaamini ugumu katika
maisha basi na ndivyo inavyokuwa.Soma; Kama Unaona Maisha Ni Magumu Utawezaje Kushinda?
Acha kuamini sana maisha yako ni magumu. |
2. Kuahirisha mambo mara kwa mara.Pia
wengi wanakwama kufikia mafanikia kwa sababu ya tabia ya kuahirisha
mambo. Utakuta mtu anauwezo kabisa wa kufanya jambo fulani muda huu
lakini unashangaa anaahirisha. Kwa tabia hiyo ya kuahirisha jambo hili
leo na lingine kesho, hupelekea mambo mengi kutokufanyiwa kazi. Matokeo
yake mwisho wa siku hujikuta kukwama na kushindwa kufanikiwa. Kwa hiyo
kuahirisha mambo ni moja ya tabia inayowarudisha wengi kimafanikio bila
hata pengine wao kujua.3. Kulaumu wengine.Wapo
wengine pia ambao maisha yao hurudi nyuma kutokana na kulaumu wengine.
Unaweza ukashangaa hili linatokeaje? Sikiliza, unapolaumu wengine
unakuwa unaona wao ndio wanajukumu la kubadilisha maisha yako na kusahau
kwamba jukumu hio unalo wewe. Wewe ndio unayewajibika kwa sehemu kubwa
juu ya maisha yako na sio mtu mwngine. Kama utaendelea kulaumu wengine
ndio chanzo cha maisha yako kuwa mabaya, tambua kabisa utakuwa
umejibebesha tabia ambayo inakurudisha nyuma.Soma; Kama Unataka Mabadiliko Makubwa, Anza kubadili Kitu Hiki Kwanza.4. Kujilinganisha na wengine.Ili
uweze kufanikiwa na kufika mbali, acha kujilinganisha sana na watu
wengine. Fanya kwa sehemu yako lakini kwa ubora wa hali juu. Ikiwa
utaamua kujilinganisha sio mbaya lakini isiwe kupitiliza. Kama
utaendelea kujilinganisha sana itakupelekea uendelee kuiga maisha ya
wengine sana, ambayo kiuhalisia sio yako. Hivyo, ikiwa unataka
kufanikiwa acha kuendeleza tabia hii ya kujilinganisha sana na wengine,
itakukwamisha na utashndw kufanikiwa.Kwa sehemu hizo ni baadhi ya tabia mbovu ambazo zinawarudisha wengi nyuma kimafanikio iwe kwa kujua au kutokujua.Tunakutakia kila la kheri na ansante kwa kutembelea AMKA MTANZANIA kwa ajili ya kujifunza.Kwa makala nyingine za mafanikio pia endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.Ni wako rafiki,Imani Ngwangwalu,Simu; 0713 048035,Email;dirayamafanikio@gmail.comBlog; dirayamafanikio.blogspot.com
Article Source: Hisia za Mwananchi
Comments