Mbwana Samatta amecheza dakika zote 90 za mchezo kati yake ya Genk
dhidi ya Anderlecht na kuisaidia Genk kuibuka na ushindi wa magoli 5-2
katika kampeni za kuhakikisha timu yao inapata nafasi ya kushiriki
michuano ya Europa League.
Anderlecht walianza kufunga goli la kuongoza dakika ya 25 kupitia kwa
kiungo wao Filip Djuricic lakini goli hilo lilisawazishwa na Leon
Bailey dakika ya 45 na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko timu zote
zikiwa sare kwa kufungana goli 1-1.
Kipindi cha pili Suarez aliiweka tena mbele Anderlecht kwa kuifungia
bao la pili dakika ya 60 lakini dakika tano baadaye Buffel
aliisawazishia Genk. Dakika ya 76, Pozuelo aliiweka mbele Genk kwa
kutupia bao la tatu kisha Ndidi akaongeza bao la nne kabla ya Nikos
Karelis hajamaliza shughuli kwa kufunga goli dakika ya 90 ya mchezo.
Samatta kucheza dakika zote 90 ni faraja kubwa kwasababu mchezo
uliopita alitolewa kipindi cha kwanza wakati Genk ilipocheza na KV
Oostende.
Samatta amesema sababu kubwa iliyopelekea kushindwa kuendelea na
mchezo ule ilikuwa ni majereha aliyoyapata wakati wa kipindi cha kwanza
cha mechi hiyo.
“Mechi iliyopit nilipata majeruhi kwenye kipindi cha kwanza cha mechi
hiyo, niliumia eneo la nyonga kwa hiyo baada ya kurudi vyumbani na
kuwaeleza madaktari, waliniambia nipumzike kwasababu ningeweza kuendelea
lakini wasiwasi ukawa ni kwamba huenda majeraha yangeongezeka halafu
ingechukua muda zaidi kupona”.
“Kwahiyo madaktari waliamua nipumzike baada ya kupata maumivu,
madaktari walijitahidi nipone haraka kwa ajili ya mchezo wa leo na jana
nilifanya mazoezi pamoja na timu, kucheza au kutocheza kwenye mchezo wa
leo ilikuwa ni mipango ya mwalimu.”
Endapo Genk watashinda mchezo wao wa mwisho siku ya Jumapili,
watafuzu moja kwa moja kucheza Europa League lakini kama watamaliza
wakiwa nafasi ya nne basi watalazimika kucheza play off nyingine dhidi
ya mshindi wa play off II kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya
Europa.
Comments