Msanii wa filamu nchini Rose Ndauka ameweka wazi kuwa kwenye tasnia
hiyo wapo baadhi ya watu wachache ambao wameingia kwenye tasnia hiyo
wakiwa na lengo la kujiuza na kupata wanaume, ambao wamekuwa wakiichafua
tasnia hiyo.
Kupitia kipindi cha Mkasi, Rose Ndauka aliweka sawa kuwa kuna wasanii
ambao wanaingia kwenye tasnia hiyo kuwa kuwa wana vipaji na wanataka
kufanya filamu kama kazi na kusema wapo baadhi ambao kweli wameingia
kwenye filamu ili kupata wanaume au mabwana kupitia tasnia hiyo.
“Kiukweli si kila msanii anayeingia kwenye filamu anataka kupata
wanaume japo wapo baadhi ya watu wanasukumwa na hiyo hali lakini ukweli
ni kwamba wapo wasanii ambao wanaingia kwenye filamu sababu wana vipaji
na wanataka kufanya filamu kama kazi na kufanikiwa kimaisha” alisema
Rose Ndauka.
Mbali na hilo msanii huyo alisisitiza kuwa kitendo cha wanawake
kujiuza ni si kwenye tasnia ya filamu tu hata katika maisha ya kawaida
watu hao wapo hivyo amedai hali hiyo ni hulka ya mtu mwenyewe na si
kutokana na kazi anayofanya au kwa kuwa yupo kwenye filamu kama ambavyo
watu wanadhani.
Comments