Kuna utata kuhusu ni nani alimuokoa na jina la msichana ni lipi.
Kumezuka
utata kuhusu msichana wa Chibok ambaye aliokolewa nchini Nigeria. Kwanza
jeshi linasema kuwa ndilo lilimuokoa msichana huyo aliyetjwa jina kuwa
Falmata Mbalala.
Hata
hivyo wanaharakati na viongozi wa kijamii wanasema kuwa msichana
aliyeokolewa, jina lake ni Amina Ali Nkek na kuwa alipatikana katika
msitu wa Sambisa na kundi la vijana na kudumisha usalama.
Msitu huo ndio maficho makuu ya wanamgambo wa Boko Haram.
Mwenyeki
wa chama cha wazazi wa Cibok mjini Abuja Hosea Abana Tsambido aliiambia
BBC kuwa vijana hao walikuwa na habati kubwa kumpata msichana huyo.BBC
Comments