Vilabu vya Chelsea na Tottenham wamepigwa faini kwa pamoja na
shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kukabiliwa na makosa matatu
ya kushindwa kuwazuia wachezaji pamoja na maofisa wake wakati na baada
ya mchezo wa jumatatu.
Kiungo wa Spurs Mousa Dembele amekumbana na adhabu pia ya kusababisha
vurugu katika mchezo huo ulioisha kwa suluhu ya 2-2.FA inasema kuwa
kitendo cha Dembele kumuingizia vidole machoni mchezaji wa Chelsea Diego
Costa ni utovu mkubwa wa nidhamu.
Hiyo ina maana ”akikutwa na hatia” kufungiwa michezo mitatu pekee
haitoshi.Dembele, 28,amepewa mpaka siku ya Alhamisi kujibu mashataka
hayo huku kwa pamoja Chelsea na Tottenham wakipewa mpaka siku ya
jumatatu.
Katika mchezo huo zilitolewa kadi za njano 12 kutokana na vurugu
zilizosababishwa na pande zote mbili. Spurs walihitaji kuifunga Chelsea
ili kuweza kurudisha matumaini ya kutwaa taji la ligi kuu England lakini
wakaishia suluhu hivyo Leicester kuwa mabingwa.
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino aliingia uwanjani kwa hatua
kadhaa kwa lengo la kuwaachanisha mlinzi wa Spurs Danny Rose na kiungo
wa Chelsea Willian,huku pia Rose akihusishwa katika tukio
lililosababisha mejena wa Chelsea kuangushwa chini.
Mwamuzi wa mchezo huo Mark Clattenburg hakuweza kutoa adhabu kwa
Dembele kwa vitendo vyake lakini kamera za uwanjani zilimnasa Mbelgiji
huyo akiingiza vidole vyake kwenye macho ya Costa.
Source: BBC
Comments