Shamrashamra zimemalizika katika mji wa Milan na badala yake sherehe
hizo za kushangilia ubingwa zimehamia kwenye jiji la Madrid ambako Real
wanasubiriwa kupokelewa na mashabiki wao baada ya kufanikiwa kutwaa taji
la vilabu bingwa barani Ulaya.
Baada ya mchezo kumalizika, makocha wote wawili walikuwa na mitazamo
tofauti kutokana na timu zao zilivyocheza na matokeo yaliyopatikana
baada ya mechi kumalizika.
Zidane yeye amefanikiwa kubeba taji hilo akiwa kocha wa saba kati ya
wale ambao waliwahi kutwaa kama wachezaji na baadaye kutwaa taji hilo
wakiwa makocha. Zidane ametumia muda mfupi sana kuiwezesha Madrid
kushinda Champions League ukilinganisha na watangulizi wake. Ndani ya
mezi sita amefanikiwa kutwaa taji hilo tangu alipokabidhiwa timu toka
mikononi mwa Rafael Benitez.
Amesema siri kubwa ya mabadiliko na mapinduzi aliyoyafanya kwenye
kikosi cha Real ni kuwasisitiza wachezaji wake kupambania mafaniko bila
kuchoka na kikubwa ni falsafa yake ya kwamba, ukifanya kazi kwa jitihada
utapata matokeo unayoyataka.
Amewashukuru wachezaji wake kwa umoja ambao wameuonesha na namna
ambavyo waliweza kupambana na kuweza kufanikiwa kushinda taji hilo.
Kwa upande wa Diego Simeone ‘El Cholo’ yeye anasema wamefeli wao kama
Atletico kwa kushindwa kubeba taji hilo licha ya kuingia kwenye fainali
mara mbili. Lakini kikubwa ambacho kimemuumiza na kumsikitisha ni pale
anapowafikiria mashibiki ambao mara zote wamelipa fedha zao kwenda
kuishuhudia timu yao mara zote inapocheza katika fainali.
Lakini akasema anawashukuru mashabiki na anajivunia wachezaji wake
kwa namna ambavyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha timu inapat matokeo.
Kuhusu mustakabali wake wa bada, Diego Simeonehajazungumza lolote.
Amesema kwa sasa ni muda wa kupumzika na kutuliza akili ili kuangalia
namna ambavyo wanaweza kuja katika msimu unaokuja.Source Shaffih Dauda
Comments