Msanii
Snura ambaye video ya wimbo wake wa mpya ‘Chura’ umefungiwa na serikali
kutokana na kutokuwa na maadili na kukiuka utamaduni wa kitanzania
amefunguka na kusema kuwa yeye kukata viuno amejifunzia kwenye ngoma za
asili.
Snura amefafanua na kuomba radhi kwa watanzania kutokana na video yake hiyo kutokuwa na maadili na kuwadhalilisha wanawake.
Snura amefafanua na kuomba radhi kwa watanzania kutokana na video yake hiyo kutokuwa na maadili na kuwadhalilisha wanawake.
“Mimi ni mwanamke na niliwachukua wanawake wenzangu kucheza lakini haina maana kuwa niliwachukua ili niwadhalilishe hapana, ila nakiri kuwa nilichokosea ni kuwaingiza kwenye maji ndiyo maana ilionekana kama ni udhalilishaji kwao. Lakini kucheza hakumdhalilishi mtu na ndiyo maana kuwa bendi wachezaji show wake wanakatika hata kwenye ngoma zetu za asili tunakatika, mimi nimejifunza kukatika kwenye ngoma za asili kwani ndiyo kipaji changu cha kwanza na huko ndiyo nimejifunzia kiuno” alisema Snura
Comments