Shamrashamra zimemalizika katika mji wa Milan na badala yake sherehe hizo za kushangilia ubingwa zimehamia kwenye jiji la Madrid ambako Real wanasubiriwa kupokelewa na mashabiki wao baada ya kufanikiwa kutwaa taji la vilabu bingwa barani Ulaya. Baada ya mchezo kumalizika, makocha wote wawili walikuwa na mitazamo tofauti kutokana na timu zao zilivyocheza na matokeo yaliyopatikana baada ya mechi kumalizika. Zidane yeye amefanikiwa kubeba taji hilo akiwa kocha wa saba kati ya wale ambao waliwahi kutwaa kama wachezaji na baadaye kutwaa taji hilo wakiwa makocha. Zidane ametumia muda mfupi sana kuiwezesha Madrid kushinda Champions League ukilinganisha na watangulizi wake. Ndani ya mezi sita amefanikiwa kutwaa taji hilo tangu alipokabidhiwa timu toka mikononi mwa Rafael Benitez. Amesema siri kubwa ya mabadiliko na mapinduzi aliyoyafanya kwenye kikosi cha Real ni kuwasisitiza wachezaji wake kupambania mafaniko bila kuchoka na kikubwa ni falsafa yake ya kwa...