MWENYEKITI
wa Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba, Jaji
Joseph Warioba amevitaka vikundi na wananchi waliopendekeza wajumbe wa
Tume hiyo, kuiacha ifanye kazi iliyopewa kufanya.
Pamoja na hayo, Tume hiyo jana ilikabidhiwa rasmi jengo la ofisi ya kufanyia kazi, kuahidiwa magari 30, kuajiri watumishi wa sekretarieti watakaosaidia na kuanzishiwa fungu maalumu la kuiwezesha kufanya kazi.
Akizungumza wakati Tume hiyo inakabidhiwa ofisi Dar es Salaam, Jaji Warioba ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu, alisema waliopendekeza majina ya wajumbe hao, wasitarajie kuwa wajumbe hao watafanya watakavyo wao kwani Tume hiyo ni ya Watanzania wote na si watu wachache.
“Naomba kwa dhati kabisa, waliotupendekeza watuache tufanye kazi, tumepewa jukumu la nchi tuacheni tufanye kazi bila shinikizo,” alisema Jaji Warioba.
Alisema iwapo waliopendekeza Tume hiyo wanadhani kuwa wameweka watu wao hivyo mambo yatafanyika kama wanavyotaka wao, watakuwa wanajidanganya kwa kuwa kazi ya Tume ni moja tu ya kutumikia wananchi.
Alisema majukumu ya Tume hiyo si kuandika Katiba bali kukusanya maoni, kuyachambua na kuandika rasimu ya Katiba ambayo itazaa Katiba mpya.
Alihamasisha wananchi kujiandaa na kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao. Alisema Tume hiyo iliyoanza kazi juzi, inaandaa utaratibu utakaoiwezesha kufikia wananchi wengi ili kupata maoni mengi.

Comments