MBUNGE WA CHAMA TAWALA NCHINI MAREKANI AHAMASISHA UANZISHWAJI WA KAMATI NDOGO (CAUCUS) YA WABUNGE KUISEMEA TANZANIA
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar
akiwa na Mhe. Dan Boren, Mbunge wa Bunge la Marekani kutoka
Oklahoma,aliyemtembelea ofisini kwakwe.
Mhe.Balozi
Maajar akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge Dan Boren,Mkurugenzi wa
Bunge, Bi.Hilary Moffett,na kushoto na kulia na Bibi Lily Munanka Mkuu
wa Utawala Ubalozini na Afisa Ubalozi Bw. Suleiman Saleh.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar,Jumatano Mei 9, 2012 alimpokea Ubalozini, Mhe. Dan Boren na kufanya naye mazungumzo ya uanzishwaji wa Tanzania Caucus katika Bunge la Marekani ambapo Tanzania itakuwa imepata mtetezi na msemaji bungeni humo kila linapotokea jambo linalohusu Tanzania.
Mhe. Boren ni mbunge wa Bunge la Marekani kutoka Wilaya ya Pili, Jimbo la Oklahoma, amehamasisha na hatimaye kuanzisha kundi la wabunge wenye mapenzi na Tanzania, kamati ndogo (caucus) ya kuisemea Tanzania kwenye Bunge la Marekani.
Mhe. Boren ambaye ni mbunge kutoka Chama Tawala cha Democrat ameasisi Kundi hilo hilo akishirikiana na wabunge wenzake kadhaa wa chama chake na wengine kutoka Chama cha Republican kutokana na kufurahishwa kwao na juhudi za Serikali ya Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kuimarisha demokrasia, utawala bora pamoja na juhudi za kimaendeleo katika sekta za uchumi, nishati, kilimo na hifadhi ya mazingira.
Katika ziara yake hapa ubalozini Mhe. Boren aliyeambatana na Bi. Hilary Moffett, Mkurugenzi wa Sheria Bungeni, alimhakikishia Mhe. Balozi Maajar utayari wake wa kuisaidia Tanzania katika juhudi zake hizo.
Aidha alibainisha kwamba Tanzania ina changamoto nyingi sana mbele yake na hivyo kuwepo kwa sauti mpya ya kuisemea katika Bunge la Marekani ni jambo ambalo analiona litakuwa na manufaa makubwa kwa nchi.
Sambamba na hilo, Mhe. Boren alibainisha kwamba Tanzania imekuwa ni moja ya nchi ambazo Serikali ya Marekani inaziangalia kwa umakini kama mfano wa nchi bora na hivyo ameona ni vyema naye akaunga mkono juhudi hizo za Serikali ya Rais Barack Obama.
Kwa upande wake, Mhe.Balozi Mwanaidi Sinare Maajar alifurahishwa na kufarijika na ujio wa Mhe. Boren Ubalozini na kumueleza kwamba atashirikiana naye bega kwa bega na kuahidi kwamba muda wowote atakapohitajika kukutana na kamati hiyo ya Bw. Boren yupo tayari.
Mhe. Maajar alimshukuru Mhe.Boren kwa mwaliko wake kutembelea Jimbo la Oklahoma ili Tanzania ipate kueleweka zaidi na hivyo kufungua pazia la ushirikiano katika sekta mbali mbali za Uchumi, Kilimo, Nishati na Utalii

Comments