BONDIA
Floyd Mayweather Jr. ameendeleza ubabe baada ya alfajir hii kumtandika
kwa pointi Miguel Cotto katika pambano lililokuwa kali na la kusisimua.
Mayweather
alitumia kasi yake na ufundi kumshinda Cotto, ingawa haikuwa kazi
nyepesi kwani mpinzani wake huyo alikuwa akitupa makonde ya maana na
kushambulia mwanzo mwisho.
''Wewe
ni bingwa hatari,'' Mayweather alimuambia Cotto ulingoni baada ya
pambano. 'Wewe ni kinana wa nguvu ambaye sijawhai kukutana naye.''
Mayweather
alitawala raundi ya mwisho, ya 12 akimnyanyasa Cotto na kujihakikishia
kucheza mapambano 43 bila kupigwa. Tofauti na mapmabano yake mengi,
Mayweather alitokwa damu puani mbele ya Cotto.
Majaji wawili walitoa pointi 117-111 na wa tatu akatoa 118-110, hivyo Mayweather ameshinda kwa pointi 116-112.
Mayweather
aliyepigana wiki chache tu kabla ya kuingia jela ya kutumikia kifungo
cha miezi mitatu, alikutana na pambano gumu dhidi ya mplnzani ambaye
anakwenda mbele wakati wote.
Lakini alikuwa mwenye kasi na mjanja zaidi ya Cotto na alionekana kumvaa katika raundi za mwisho.
Katika
raundi ya mwisho, Mayweather alipiga ngumi yake bora zaidi kwenye
pambano hilo, uppercut ya mkono wa kushoto ambayo ilimuonekana kumuumiza
Cotto.
Mayweather,
aliyeahidiwa kupewa dola za Kimarekani Milioni 32, alilazimika kupigana
kila dakika katika raundi 12 za pambano dhidi ya mbabe huyo wa Puerto
Rico.
Mayweather
atakuwa jela wakati Manny
Pacquiao anapanda ulingo huo huo wa MGM Grand Juni 9, dhidi ya Timothy
Bradley.
Pambano tamu zaidi la ngumi wanalolisubir9ia wapenzi wengi wa
mchezo huo duniani ni kati ya Mayweather dhidi ya Pacquiao, ambalo
halijapangwa kufanyika.
Hii
inatokana na msistizo wa Mayweather kutaka Pacquiao afanyiwe vipimo vya
kutumia dawa za kuongeza nguvu, ingawa tayari Pacquiao amesema yuko
tayari kufanya hivyo.
''Nataka
kupigana na Pacquiao, lakini anahitaji kufanyiwa kwanza vipimo vya
kutumia dawa za kuongeza nguvu kabla ya kupambana naye,'' alisema
Mayweather.
Takwimu za makonde, zinaonyesha Mayweather alipiga ngumi 179 zilizofika kati ya 687 alizotupa na Cotto alipiga ngumi 105 zilizofika kati ya 506.
Cotto,
ambaye sasa anakuwa amepigwa mapambano matatu 37, aliahidiwa kupewa dau
kubwa zaidi katika historia yake ya kupigana, dola Milioni 8.
Comments