Tunapenda
kuwatarifu wadau wetu wote wanaoishi DMV na vitongoji vyake kwa wale
wanaopenda mchezo wa kandanda, timu ya taifa ya Marekani itakuwa
mwenyeji wa Brazil katika mechi ya kirafiki itakayochezwa, Mei 30 mida
ya 8 p.m. ET, hapa hapa FedExField Landover, Maryland.
US itatakuwa nimara ya pili
kukutana na Brazil tangu kusimamuwa na kocha mzowefu kutoka Ujerumani
Jurgen Klinsmann siku hiyo ya Mei 30.
"Unapozungumzia kuhusu Brazil,
unazungumza kuhusu kandanda na wengi wenye vipaji kucheza katika taifa
ambalo linajulikana duniani," alisema kocha mkuu wa Marekani Jurgen
Klinsmann kwenye ussoccer.com. "Ni lengo letu kuwa na tuna uwezo wa
mechi za juu dhidi ya timu kama Brazil ndani ya msingi imara, na hii ni
nafasi ya kujimarisha zaidi.
Hii ni kuwakumbusha tu wadau
wanaotembelea blog hii, wahi tiketi yako mapema, kwa sasa zinapatikana
bei nafuu online, kabla hazijapandishwa bei wakati pale hamu imeshakujia
ya kwenda kuwaona mabingwa wenye vipaji duniani katika janga la soccer
timu ya Brazil, ambayo mechi hiyo utachezwa hapa FedExField Landover,
Maryland.
Kwa habari zaidi ya mpambano huu bofya hapa
Comments