Mapigano
yalizuka jana jioni wakati wanajeshi wa rais wa zamani Amadou Toumani
Toure walipojaribu kudhibiti televisheni ya serikali kutoka kwa
wanajeshi waliotwaa udhibiti wa kituo hicho katika mapinduzi, mwezi
Marchi.
Viongozi
wa mapinduzi hayo wamesema wanajeshi hao wa rais wa zamani pia
walijaribu kudhibiti uwanja wa ndege, ili kujiandaa kuwasili kwa jeshi
la mataifa ya magharibi, ambalo madhumani yake ni kurudisha utawala wa
kiraia. Mpango huo tayari umekataliwa na viongozi hao wa mapinduzi.
Walioshuhudia wanasema kufuatia mapigano hayo, sasa mitaa ya mji wa Bamako haina watu na kwamba umeme umekatwa katika maeneo mengi.
Televisheni ya serikali imekuwa ikipeperusha vipindi badala ya habari.
Baadhi ya ripoti zinaashiria kuwa vurugu hizo zilichochewa na jaribio la kutaka kumkamata afisa wa zamani ya rais Toumani Toure, aliyemsaidia kutoroka wakati wa mapinduzi.

Comments