Chama cha kansela Angela Merkel cha CDU kinakabiliwa na kipigo katika uchaguzi wa jimbo lenye wakaazi wengi nchini Ujerumani, la North Rhine Westphalia Jumapili (13.05.2012).
Uchaguzi huo ambao umeitishwa na mapema unaweza kutoa msukumo kwa mahasimu wakubwa kansela wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi wa kitaifa mwaka 2013.
Wiki moja baada ya wapiga kura nchini Ugiriki na Ufaransa kukataa sera za kubana matumizi, raia wa jimbo la North Rhine Westphalia (NRW) huenda wakawaadhibu wahafidhina ambao wamekuwa wakipigia upatu sera za kubana matumizi.
Waziri mkuu wa jimbo la NRW
Hannelore Kraft
|
NRW ushawishi kitaifa
Jimbo hilo kihistoria linanafasi kubwa katika siasa za shirikisho, ambapo mwaka 2005 , chama cha kansela wa wakati huo Gerhard Schroeder kilipoteza uchaguzi na kumlazimisha kuitisha uchaguzi wa shirikisho wa mapema na ndipo kansela Angela Merkel akaingia madarakani.
Chama cha kihafidhina cha kansela Angela Merkel cha Christian Democratic Union, CDU, kinapambana kukamata jimbo hilo kutoka kwa muungano unaoundwa na vyama vya mrengo wa shoto vya Social Democratic SPD na kile cha kijani.
Uchunguzi wa maoni
Licha ya uchunguzi wa maoni ya wapiga kura kuwa unaonyesha mara kwa mara kuwa chama cha Merkel kinaungwa mkono na wapiga kura wengi kwa msimamo wake wa kubana matumzi katika bara la Ulaya , chama cha CDU kiko nyuma ya SPD kwa alama sita hadi saba katika maoni ya wapiga kura katika jimbo la NRW.
Comments