Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa (AFDB) Bw. Ngosha
Magonya katikati akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini
Arusha.
Baadhi ya wanakamati wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa AFDBwakiwa katika viwanja vya AICC jijini Arusha leo.
NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
Benki ya maendeleo ya
Afrika (AFDB)inatarajia kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 12 katika mkutano
wake unaoanza Jumatatu jijini Arusha na kufunguliwa na Raisi Jakaya Kikwete huku kiasi cha fedha hizo zikitumika kukarabati
Kumbi mbalimbali za jengo la Kimaitaifa la ukumbi wa AICC kwa kuwa baadhi ya
kumbi za jengo hilo zinaonekana kupitwa na wakati kutokana na utandawazi uliopo
kwa sasa ndani ya nchi zilizoendelea
Akizungumza jijini hapa na waandishi wa habari mwenyekiti wa
kamati ya kitaifa ya mkutano wa benki ya AFDB kwa mwaka 2012 Bw Ngosha Magonya ambapo alisema kuwa mkutano huo utakuwa na
faida kubwa sana
Alifafanua kuwa kupitia mkutano huo ambao utaanza Jumatatu ijayo
utakuwa na faida kubwa sana kwa jiji la Arusha kwa kuwa hata kiwango cha uchumi
kitaaimarika sana kwa kuwa wageni mbalimbali kutoka katika maeneo ya nchi
mbalimbali duniani watabadilishana hata uzoefu
“kwa kipindi hiki ambacho kuna mikutano ndani ya jiji la
Arusha tunatarajia kuwepo na utoafuti wa khali ya juu sana hasa katika mchakato
wa uchumi na kwa hali hii pia tunatarajia hata kufanya maendeleo
mbalimbali ikiwemo kufanya marekebisho
kwa jengo la kimataifa la AICC”alisema bw Magonya
Katika hatua nyingine alifafanua kuwa mbali na kuweza kuimarisha
uchumi wa mkoa wa Arusha pia wanatarajia kutumia fursa mbalimbali za
kuhakikisha kuwa wanakutanisha wafanyabiashara mbalimbali huku malengo yakiwa
ni kuendeleza uchumi kwa walengwa.
Pia alifafanua kuwa mbali na kuweza kuwasaidia
wafanyabiashara hao katika michakato ya kukuza uchumi pia benki hiyo ina
mikakati mbalimbali ya kuendeleza barabara ambazo zitaweza kutumika kama njia
ya mawasiliano hapa Tanzania hali ambayo nayo itachangia kwa kiwango kikubwa
sana hata kuimarisha uchumi wa nchi ya Tanzania
Aliongeza kuwa hapo awali benki hiyo ilikuwa imeshajenga
barabara ya Arusha –Namanga kwa sasa ana mpango wa kujenga barabara ya Arusha –
Holile ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro hali ambayo itachangia sana maendeleo hasa
ya mawasiliano
Alimalizia kwa kusema kuwa wafanyabiashara hasa wa mkoa wa
Arusha wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vema fursa za mkutano huo ili
kuweza kuimarisha biashara zao za kila siku.Inatoka kwa mdau.
Comments