Skip to main content

MAISHA MAFUPI YA STEVE KANUMBA NI STAFTAHI YA FILAMU ZETU



Nilianza kumsikia- Stephen Charles Kanumba- wakati wa joto-joto la – Big Brother  South Afrika 2009- aliposababisha mjadala mkali wa uzungumzaji wa Kiingereza, sanaa, uzalendo,nk.
Marehemu Kanumba akithibisha mapenzi ya kazi yake kwa kushikilia kamera wakati wa kutengeneza filam ndogo ya “Lovely Gamble”  Septemba 2009 na Urban Pulse, Uingereza. Nyuma ni hoteli maarufu la wana Msumbiji- “Nandos.” Picha ihsani ya Urban Pulse, Reading.
Steve Kanumba alikuwa mwigizaji wa kwanza wa Kitanzania kujitokeza nje ya Bongo na mjadala ukawa moja ya matokeo yaliyochomoza kutokana na juhudi zake kisanaa. Wapo waliomcharura kuwa hakuongea Kiingereza sawasawa na waliotetea kwamba uzungumzaji Kiingereza fasaha haukuwa muhimu kuliko kipaji na jasho la mtu. Ila la msingi ni namna alivyojitokeza haraka na kutikisa bendera ya Bongo na waigiza sinema wa Nigeria, Ghana, Afrika Kusini, nk. Continue Reading »

Comments