Release No. 069
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 8, 2012
TWIGA STARS KUJIPIMA KWA ZIMBABWE
Timu
ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) itacheza na Zimbabwe katika mchezo
wa kirafiki utakaofanyika Mei 12 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Twiga
Stars hivi iko katika ziara ya mechi za kirafiki katika mikoa ya Dodoma
na Mwanza. Leo (Mei 8 mwaka huu) itacheza na kombaini ya Mkoa wa Dodoma
ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 katika mchezo utakaofanyika
Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.
Kesho
(Mei 9 mwaka huu) itaondoka kwenda jijini Mwanza ambapo pia itacheza
mechi moja ya kirafiki Mei 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,
na kurejea Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Zimbabwe.
Zimbabwe
inatarajia kuwasili kesho (Mei 9 mwaka huu) jioni kwa ndege ya South
African Airways (SAA) ikiwa na msafara wa 25 na wataondoka Mei 14 mwaka
huu alfajiri.
KAMATI YA MASHINDANO KUPANGA VITUO LIGI YA TAIFA
Kamati
ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia
kukutana leo (Mei 8 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine itapanga
vituo vya Ligi ya Taifa na tarehe ya kuanza ligi hiyo.
Mikoa
nane imeomba kuwa wenyeji wa ligi hiyo itakayochezwa katika vituo
vitatu. Mikoa hiyo kupitia kwenye vyama vyao vya mpira wa miguu ni
Mikoa iliyoomba vituo ni Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Mara, Mbeya, Shinyanga na Singida.
Timu
zinazoshiriki ligi hiyo ni mabingwa wa mikoa. Timu hizo ni Ashanti
United ya Ilala (Dar es Salaam), Aston Villa (Singida), Bandari FC
(Kagera), CDA (Dodoma), Flamingo SC (Arusha), Forest FC ya Siha
(Kilimanjaro), JKT Kanembwa (Kigoma), Korogwe United ya Korogwe
(Tanga), Kurugenzi ya Mafinga (Iringa), Lindi SC (Lindi) na Majimaji
(Tabora).
Mighty
Elephant (Ruvuma), Mkamba Rangers ya Kilombero (Morogoro), Mpanda Stars
ya Mpanda (Rukwa), Mwadui FC (Shinyanga), Nangwa VTC (Manyara), Ndanda
FC (Mtwara), Pamba SC (Mwanza), Polisi Mara (Mara), Red Coast ya
Kinondoni (Dar es Salaam), Super Star ya Bagamoyo (Pwani), Tenende SC
(Mbeya) na Tessema FC ya Temeke (Dar es Salaam).
KILA LA KHERI SIMBA, PONGEZI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Simba
kwenye mechi yake ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly
Shandy ya Sudan itakayochezwa Jumapili (Mei 13 mwaka huu).
Mechi
hiyo itachezwa katika mji wa Shandy kuanzia saa 2 kamili usiku kwa saa
za Afrika Mashariki. Simba inaondoka kesho kwenda huko kwa ndege ya
Kenya Airways.
Msafara
wa timu hiyo utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Hussein
Mwamba, na unatarajia kurejea nyumbani Mei 15 mwaka huu.
Pia
TFF inaipongeza Simba kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) ambayo Mei 6 mwaka huu ilifunga msimu wa 2011/2012.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Comments