Skip to main content

John Mnyika:"Toa Kitabu Kisomwe"-Mimi Nimeanza,Wewe je?


 Mbunge wa Jimbo la Ubungho(CHADEMA)mheshimiwa John Mnyika
---
Juzi jumapili tarehe 6 Mei 2012 nimekabidhi zaidi ya vitabu mia saba (700) kama ishara ya kuanzisha Programu ya Taarifa iitwayo “Toa Kitabu Kisomwe”, hii ni miezi mitatu baada ya kusambaza kwa wananchi wa jimbo la Ubungo vitabu 4500 ikiwa ni pamoja na nakala za katiba ya nchi na vitabu kuhusu mchakato wa katiba mpya; na kufanya jumla ya vitabu ambavyo nimesambaza mpaka sasa kuwa zaidi ya elfu tano (5,000).

Lengo ya Programu ya Taarifa ya “Toa Kitabu Kisomwe” ni kusambaza jumla ya vitabu visivyopungua elfu hamsini (50,000) ndani ya Manispaa ya Kinondoni katika kipindi cha mwaka ili kuchochea uhuru wa kifikra na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

Kwa mtazamo wangu akili na vipaji ambavyo kila mwanadamu amejaliwa ndiyo mtaji mkuu wa kujikwamua kimaisha. Hivyo kushirikiana kuwezesha elimu bora na uhuru wa kifikra ni msingi muhimu wa kuchochea maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Elimu bora sio majengo pekee bali ni pamoja na walimu bora na mazingira bora ya kusomea na kujifunzia yenye vifaa vya kujifunzia na vitabu vya kiada na ziada.

Hivyo, harakati za kusimamia uwajibikaji wa serikali kuu, serikali za mitaa na mamlaka nyingine zinazohusika na sekta ya elimu hususani kwenye shule, vyuo na vyuo vikuu vya umma zinapaswa kuendelezwa.

Tuendelee kuhakikisha rasilimali zinazotengwa ikiwemo ruzuku ya elimu ya msingi na sekondari na mikopo ya elimu ya juu zinakuwa za kutosha, zinatolewa kwa wakati na zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kudhibiti mianya ya ufisadi.

Wakati, tukisimamia uwajibikaji huo wa serikali tutambue masuala matatu muhimu; mosi, jukumu la kuboresha mazingira ya elimu kwenye elimu rasmi ya darasani sio wa serikali pekee bali ni wajibu wa wote katika jamii.

Pili, izingatiwe kuwa sehemu kubwa ya wananchi hawajapata elimu rasmi hivyo ni muhimu kuwa na mifumo ya elimu kwa njia nyingine mitaani na vijijini ili kuchochea zaidi maendeleo.

Tatu, hata kwa wenye elimu rasmi inafahamika kuwa elimu haina mwisho hivyo kila mmoja ana wajibu wa kujisomea ili kuendeleza uhuru wa kifikra.

Katika muktadha wa masuala hayo matatu, niliungana na Asasi ya Maendeleo Ubungo (Ubungo Development Initiative-UDI) kuzindua Programu ya Taarifa inayohusisha kukusanya vitabu vya kiada na vya ziada kutoka wa watu mbalimbali na taasisi mbalimbali na kuvisambaza katika taasisi za elimu kwa ajili ya wanafunzi kusoma na maeneo maalumu kwa ajili ya wananchi kujisomea.

Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema kwamba ukimpa mtu samaki umemlisha kwa siku moja lakini ukimfundisha kuvua umemlisha kwa maisha yake yote. Nikisisitiza mantiki ya msemo huo naweza kusema pia kwamba ukimpa mtu chakula cha kawaida umemshibisha kwa muda mfupi lakini ukimpa chakula cha kifikra umemuwezesha kwa muda mrefu; huu ndio msingi utakaoongoza Programu ya Taarifa; “Toa kitabu kisomwe”.

Kupitia programu hii tunaomba taasisi au mwananchi yoyote mwenye kitabu chochote popote ambaye yuko tayari kukitoa ili kisomwe iwe ni cha kiada au cha ziada awasiliane UDI ili iweze kufikisha kitabu hicho kwa walengwa.

Ukipenda unaweza kuweka saini kwenye kitabu hicho kama kumbukumbu kuwa taasisi yenu au wewe ndiye uliye “Toa kitabu Kisomwe” au unaweza pia kutueleza kitabu hicho unapendekezwa kipelekwe wapi ndani ya Manispaa ya Kinondoni ili kiweze kusomwa kwa ufanisi.

Sisi mpango wetu ni kusambaza vitabu hivyo kwenye maktaba za shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu kwa upande wa elimu ya kiada na kusambaza kwenye maktaba za jumuia, ofisi za serikali za mtaa, taasisi za kijamii na vijiwe vya kudumu kwa upande wa elimu ya ziada.

Naamini kwamba kwenye kaya mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni vipo vitabu makabatini au masandukuni ambavyo ama ni vya kiada vilivyoachwa baada ya walengwa wa awali kupanda ngazi moja ya elimu kutoka ile ambayo walikuwa wakisoma au ni vya ziada ambavyo tayari wahusika walishavitumia na vinaweza kuwa na mchango mkubwa kwa walengwa wengine wenye kuvihitaji hivyo; “Toa Kitabu Kisomwe'' Kwa habari zaidi Mtembelea Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)Mh, John Mnyika kupitia

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...