Rais Barack Obama ameufungua rasmi mkutano wa mataifa yenye utajiri mkubwa wa viwanda G8 na kuungana na rais mpya wa Ufaransa kwa kuhimiza kwanza ukuaji wa uchumi badala ya kubana matumizi.
Rais Barack Obama na viongozi wa mataifa mengine yenye utajiri mkubwa wa viwanda wameweka kando majadiliano juu ya matatizo ya kiuchumi ya mataifa ya Ulaya na Afghanistan hali ambayo itatamalaki mazungumzo ya mkutano huo wa wiki nzima na kuangalia njia za kuimarisha nguvu za mataifa ya dunia dhidi ya maendeleo kuhusu silaha za kinuklia za Iran na kuhimiza jibu la nguvu zaidi katika hali ya ghasia inayozidi kuporomoka nchini Syria.
Barack Obama na Francois Hollande
|
Madeni ya Ulaya
Mkusanyiko huo wa viongozi unakuja katika kivuli cha mzozo wa madeni wa mataifa ya eneo la euro na kuporomoka kwa uungwaji mkono wa umma katika vita vya Afghanistan. Mtafaruku wa kisiasa na kiuchumi nchini Ugiriki na Hispania unaelezea jinsi vipi uchumi wa mataifa ya Ulaya ulivyo tete baada ya kuzipiga chini serikali zinazoshabikia ubanaji wa matumizi.
Waziri wa fedha wa Ujerumani ametabiri siku ya Ijumaa kuwa mzozo huo unaweza kuwepo kwa muda wa miaka miwili mingine.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel atakabiliwa na msukumo kutoka kwa Obama na rais mpya wa Ufaransa Francois Hollande kuchukua hatua zaidi zenye lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi.
Comments