Skip to main content

Lady Gaga:Nahitaji kufundishwa mambo ya chumbani




  NEW YORK,Marekani

MWANAMUZIKI Lady Gaga amesema kuwa tofauti na unavyomzania kama ni mtukutu katika masuala ya chumbani,lakini juzi aliweka wazi kwamba anahitaji mtu wa kumuelekeza  kuhusu masuala hayo.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun mwanadada huyo aliweka wazi  taarifa hizo juzi wakati alipohojiwa kuhusu kitu kinachomsumbua kichwa katika  maisha yake  ambapo alisema kwamba suala la chumbani ndilo bado anahitaji kupewa darasa.
 Kwa jinsi nilivyo nadhani kila mmoja anafikiri  mimi ni mtukutu katika masuala ya chumbani, lakini siyo nadhani nitafurahi jambo hilo  hapo  nitakapokuwa mkubwa,alisema.

Miaka michache iliyopita nyota huyo hajawahi kuwa na mahusiano ya  muda mrefu na mwanamume yoyote baada ya kuwa na mahusiano ya mfululizo  na  vijana kadhaa ambao hata hivyo wamekuwa wakimuacha njia panda.

Akizungumzia kuhusu hali hiyo mwanadada huyo alisema : “Nimewahi kuwazimia wanaume wengi wenye umri mkubwa   na baadaye nilipata wakubwa zaidi na ambao wamepevuka,lakini  kazi yangu ikawa ni muhimu kuliko kitu chochote,".

“Kila mmoja ambaye amekuwa akiingilia  maisha yangu nimekuwa nikimpiga kibuti na kuelekeza jitihada zangu kwenye muziki na hadi sasa mapenzi ndicho kitu ambacho kinanisumbua katika maisha yangu,"alisema.

.
 

Comments