Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa (AFDB) Bw. Ngosha Magonya katikati akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Arusha. Baadhi ya wanakamati wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa AFDBwakiwa katika viwanja vya AICC jijini Arusha leo. NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB)inatarajia kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 12 katika mkutano wake unaoanza Jumatatu jijini Arusha na kufunguliwa na Raisi Jakaya Kikwete huku kiasi cha fedha hizo zikitumika kukarabati Kumbi mbalimbali za jengo la Kimaitaifa la ukumbi wa AICC kwa kuwa baadhi ya kumbi za jengo hilo zinaonekana kupitwa na wakati kutokana na utandawazi uliopo kwa sasa ndani ya nchi zilizoendelea Akizungumza jijini hapa na waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya mkutano wa benki ya AFDB kwa mwaka 2012 Bw Ngosha Magonya ambapo alisema kuwa mkutano huo utakuwa na fai...