na mharifu aliyepindukia wa nchini Kolombia, huyu alifahamika kwa jina la Pablo
Emilio Escobar Gaviria, alizaliwa Desemba 1, 1949 na kuuawa Desemba 2, 1993.
Alikuwa ni mzaliwa wa Kolombia aliyekuwa maarufu duniani kutokana na vitendo vyake
vya kiharifu na kujihusisha kwa kiasi kikubwa katika biashara ya dawa za kulevya
zilizompatia utajiri mkubwa hadi kutangazwa na jarida la Forbes kuwa ni tajiri wa
saba duniani, mwaka 1989.
Baba yake Escobar alikuwa ni mkulima na mwalimu wa shule, wakati akiwa na miaka
miwili familia yake ilihamia kitongoji cha Envigado, katika jiji la Medellin, nchini
Kolombia.
Escobar aliwahi kusoma katika chuo kikuu cha Universidad de Antioquia,
akisomea sayansi ya siasa, hata hivyo hakuwahi kumaliza masomo yake kutokana
na kushindwa kulipa ada ya masomo yake.
Kabla ya kujiingiza rasmi katika biashara ya cocain, Escobar alikuwa akiiba
magari mjini MedellÃn, Colombia, wakati huo alikuwa chini ya miaka 19.
Mbali na shughuli hiyo, mfalme huyo wa cocain 'King of Coca' alikuwa akiiba
mawe maalum ya kwenye makaburi (huwekwa mbele ya kaburi kuonesha upande ambao
kichwa cha marehemu kimeelekezwa), aliyasafisha vizuri na kuyauza tena kwa wateja
kutoka maeneo ya kijiji cha Antioquia na mengine kupeleka Panama.
Comments