ALIKAA miaka sita FM Academia akapata mchongo hivikaribuni mwishoni tu, mwa mwaka jana
jina halisi anaitwa Said Mtyanga alipokuwa ndani ya FM Academia alipewa jina la 'Matonge'
aliye simama kutoka kushoto (Pichani) na alipewa jina hilo kutoka kwa kingozi wa bendi hiyo Nyosh El Saadat na kulia ni msanii H Baba .
Alitimukia Oman na akiwa uko alifanya shoo za maana nakujipatia kipato kupitia Hotel
zenye umaarufu .
Aliimba uko ughaibuni takribani miezi miwili, na baadaye mwisho huo huo wa mwaka jana
akatia timu ( DRC), kwa sasa ametua na kujikita Twanga Pepeta .
Na jumamosi ya wiki iliyopita alifanya makamuzi ya maana akiwa na bendi hiyo mpya, kwa
harakati za muziki wa dansi hapa nchini kumekuwa na mashindano ya juu sana kati ya bendi ya
FM Academia na Twanga Pepeta kuna hali ya juu katika ushindani wao huku kila bendi ikikamua
kwa manufaa .
Bendi nyingine ni Acudo inayofanya makamuzi yake mara kwa mara Msasani Beach Club na
inawapenzi wake wengi tu katika jiji hili la maraha Dar es Salaam.
Comments