WIZARA ya Viwanda na Biashara imesema kuwa kuwepo kwa viwanda
vidogo (SIDO) katika maeneo mengi nchini kutasababisha uzali
shaji mkubwa wa ajira.
Hayo yameelezwa jana na Naibu Waziri wa wizara ya Viwanda na Biashara Inginia Stellah Manyanya alipofanya ziara ya kushitukiza katika ofisi ya SIDO mkoa wa Dar es Salaam iliyopo eneo Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Amelitaka Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) kuanziasha kliniki ya viwanda na biashara katika Ofisi za shirika hilo kote nchini.
Akizungumzia kuanzishwa kwa kliniki hiyo ambayo tayari Shirika hilo liliizinduwa wakati wa maonesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yaliyofikia kilele chake hivi karibuni uwepo wake katika ofisi za SIDO utaongeza ufanisi.
“Hamna budi kuanzisha kliniki hapa SIDO na mikoani ambapo SIDO inafanya kazi kwakufanya hivyo mtakuwa mmeimarisha ubora wa bidhaa kabla ya kuingia sokoni.Alisema Ijinia Stellah.
Ijinia Stellah alisema kuwepo kwa viwanda vidogo kunasababisha
wingi wa ajira unaweza ukakuta kiwanda kikubwa kikawa akisasabishi ajira ya watu wengi lakini uwepo wa viwanda vidogo katika maeneo ya kila almashauri nchini itakuwa
ni kichocheo kikubwa cha ajira.
Alisema kuwa kliniki zitahusisha wataalamu wa maabara,TFDA na TBS hivyo kurahisisha utendaji kazi kwakuwa watakuwa eneo la viwanda tofauti na sasa ambapo TBS na TFDA huwatembelea wasindikaji na wenye viwanda.
Naibu Waziri huyo alipotembelea viwanda hivyo vidogo na karakana ya SIDO alivutiwa na hali ya usafi nakuwaeleza watendaji wa SIDO na wasindikaji wa bidhaa mbalimbali kuwa wasafi zaidi nakuzingatia ufungashaji wenye mvuto.
“Ufunghashaji na uwandaaji wa lebo zitakazo vutia wateja na kuuzika kwa bidhaa zenu.Alisema Injinia Stellah.
Wakati huo huo Naibu Waziri huyo alimuagiza Meneja SIDO mkoa wa Dar es Salaam,Mackdonald Maganga kuwasiliana na Brela ili wapeleke wataalamu watakaofundisha wajasiriamali masuala mbalimbali ya usajili wa biashara zao.
Baadhi ya wajasiriamali walimueleza Naibu Waziri kuwa mitaji kwao bado ni kikwazo katika kuendeleza viwanda vyao na biashara kwa ujumla.
Naibu waziri aliwahakikishia kuwa mikopo itatolewa kwakipaumbele cha wajasiriamali waliopitia SIDO hivyo wasiwe na shaka.
Wakati huyo Meneja wa SIDO Mkoa wa Dar es Salaam Mackdonald Maganga amemhakikishia Naibu Waziri kuendeleza na kuimarisha sekta ya biashara na viwanda kwakushirikiana na Taasisi za utafiti,TBS na TFDA.
Comments