Skip to main content

TRA:Kuwasamehe wafanya biashara wenye malimbikizo makubwa

MAMLAKA ya Mapato nchini(TRA) imesema kuwa imewasamee  kodi wafanya
biashara  wenye malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma
yakijumuisha riba na adhabu .

Picha inayohusiana
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya marekebisho 
kupitia sheria yafedha  ya mwaka 2018 na sheria ya usimamizi wa
Kodi ya  MWAKA 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Kamishna Mkuu
Mamlaka ya Mapato Tanzanai Charles Kichere alisema katika marekebisho 
hayo Waziri mwenyedhamana  ya fedha na mipango  amepewa mamlaka ya
kutoa utaratibu maalum wa kuwezesha Kamisna Mkuu kutoa msamaha
riba  na adhabu  wa  hadi asilimia mia moja riba na adhabu kwenye
malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia mia moja tofauti  na
aslimia  moja tofauti na asilimia 50 ya hapo awali.

Alisema lengo kuu la msamaha huo ni kutoa unafuu kwa walipapa kodi
wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kuwapa  fursa ya kulipa
malimbikizo ya madeni  ya msingi  kwa awamu  ndani ya mwaka wa fedha
2018 hadi mwakani 2019 ili kuwapa motisha ya kulipa kodi kwa hiyari na
wakati.

"Msamaha wa riba na adhabu utahusu kodi zote zinazotozwa  kwa mujibu wa sheria
zinazosimamiwa na mamlaka ya mapato Tanzania,isipokuwa,ushuru wa forodha
unaosimamiwa chini ya sheria ya ushuru wa forodha ya jumuiya ya Afrika
Mashariki ya mwaka 2004,"alisema  Kichere.


Kichere alisema katika makato mengine  yasiyo ya kodo ambayo TRA imepewa jukumu
la kisheria la kuyakusanya mapato hayo ni kama vile kodi za majengo na ada za
matangazo ambapo walipa kodi watakaonufaika na utaratibu huu watatakiwa kuwa na
sifa  zifuatazo wawe  wamewasilisha  ritani za kodi lakini bado wanadaiwa
kodi yote au sehemuya kodi zitokanazo na ritani hizo.

Aidha alisema hata hivyo msamaha utatolewa kwa maombi yatakayokidhi mashart
na kukubaliwa na Mamlaka ya Mapato ambapo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania na Mlipakodi husika watasaini mkataba wa makubaliano utakaoainisha
deni lote la kodi.

Pia riba na adhabu inayosamehewa  pamoja na kodi iyoyo na riba wala adhabu
itakayopaswa kulipwa kabla ya tarehe 30 juni 2019.

TRA inawahimiza walipakodi wote kutumia fursa hiyo adhimu kwa kushiriki
kikamilifu katika zoezi hili maalum la utoaji wa msamaha wa riba na adhabu
ambnapo utoaji wa taarifa sisizo sahihi ni kosa kisheria na kuwa endapo
itabainika hivyo itapelekea muombaji kupoteza sifa ya kufaidika
na msamaha huo.

Comments