WADAU wa filamu nchini wameombwa kuupokea vyema ujio wa filamu ya
'Sumu' iliyoandaliwa kitaalam ikiwa na lengo lake kuelimisha jamii .
Ujio huo umeonekana kutengenezwa katika kiwango cha kimataifa na ni
mojaya sinema zenye kuleta ushindani.
Akizungumzia ujio huo jijini Dar es Salaam mtayarishaji mkuu wa filamu hiyo Hashir Khalfan
‘Kalembo’ameliambia gazeti hili kuwa filamu hiyo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza Julay 21.
mwaka huu Century Cinema, Mlimani City chini ya kampuni ya Third Eye Africa iliyoandaa uzinduzi huo.
Hashir alisema umekuwa ni utambulisho wa filamu mkubwa kwani filamu hiyo imetengenezwa
Kimataifa imeonesha weledi wa hali ya juu katika utengenezaji wake lengo ikiwa kufikisha
ujumbe kwa jamii husika.
"Filamu ya Sumu imelenga kutoa hamasa kwa watanzania kuziona filamu
za kitanzania na zile zinazotumia Lugha ya Kiswahili pekee ili kutoa fursa
kwa vijana na jamii husika kwa ujumla kutumia njia rahisi na kurejea utamaduni
wa kuangalia filamu katika majumba ya sinema (Theatre.) alisema Hashir .
Alisema baada ya kutapata hadithi ya filamu hiyo ilinichukua mudu sana kufanya
utafiti katika kupata Location sahihi kwa kazi husika,mavazi ubunifu
wa vitu mbalimbali umeifanya filamu kuwa ya kipekee na kuwa huo ni mwanzo tu
atafanya makubwa zaidi katika tasnia ya filamu
Aidha alisema kuwa filamu hiyo imelenga ushindani katika fani ya uigizaji inayotoa
nafasi kwa wasanii chipukizi kuonyesha uwezo katika sinema ya Sumu iliyotawaliwa na
Uhalisia kulingana na Hadithi.
Ujio huO umefanyika kwabajeti kubwa kulingana na kila kilichotakiwa
kilitafutwa kuanziz mavazi maalum,katika kuhakikisha sinema hiyo inaendana na
uhalisia kwani pia ni njia mojawapo katika kuleta ushindani nje ya mipaka ya Tanzania kwa watengenezaji washindani na Bongo movie.
Pia filamu imeelezwa itatengeneza njia mpya ya usambazaji kupitia Runinga ya Azam Tv kwa malipo ya Tshs. 1,000/ (Pay per View) na baadae kampuni hiyo itaangalia njia sahihi ya usambazaji ambao kila mtu ataweza kufikiwa na huduma hiyo ili aweze kufaidi kazi bora yenye
viwango vya kimataifa.
“Filamu ya Sumu ina upekee wa aina yake kwani kuna Lugha nyingi zimetumika
kama Lugha Mama ya Kiswahili na Kiarabu, ikiwa sambamba na kurekodiwa katika
nchi mbalimbali kama Sudan, Tanzania na wasanii wakali ,” alisema Hashir.
Filamu ya Sumu imerekodiwa katika nchi zifuatazo Sudan, Mombasa,
Lamu nchini Kenya, kwa Tanzania ,sinema imererkodiwa Kisiwa cha Mafia,
Arusha, Morogoro, Tanga na Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Third Eye africa Hashir ameeleza kuwa katika kuzingatia
maendeleo ya tasnia ya filamu ni lazima kuwe na njia rahisi kwa mtazamaji kufikiwa
alipo, mtu ataweza kuangalia sinema ya Sumu popote alipo kwa kutumia Azamtv
kuangalia filamu ya Sumu na kuchangia kwa gharama ndogo tu Tshs. 1,000/ na
kuona filamu yote.
Filamu ya Sumu imeshirikisha wasanii wengi hasa wachanga wapatao mia
moja ambao wana vipaji wakiwa na wasanii nguli Salim Ahmed (Gabo Zigamba),
Jennifer Temu, Hashir Khalfan na kuifanya sinema kuwa bora zaidi na imeongozwa
na Patrick Komba ambaye pia ndio mwandishi wa filamu.
Comments