KUNDI jipya katika muziki wa Bongoflava liitwalo 'Mng'ao Bandi',linalopatikana Jijini Dar es Salaamlimeanza kusambaza wimbo
wake uitwao'Maya'ukiwa umelenga kuelimisha jamii juu ya mabinti
wenye tabia mbaya kwenye mtazamo wa jamii.
Hayo yamesemwa jana na prodyza aliyehusika kutengeneza
wimbo huo Jumanne Chewe ama maarufu kwa jina la Man Jay chini ya studio yake iitwayo Lady Records maeneo ya Kigogo jijini hapa.
"Naamini kupitia muziki wao vijana hawa watapata mafanikio
kwa kuwa jamii kwa sasa imekuwa ikiwapokea vizuri wasanii wanao
ibukia kivingine katika namna ya muziki mpya,"alisema Man Jay .
Man Jay alisema kuwa kundi hilo la Mng'ao lilianza kusambaza
wimbo wao huo uitwao Maya wiki iliyopita na tayari wamefanikiwa
kufanya shoo ya kwanza katika mji wa Morogoro.
Man Jay ametaja majina ya wasanii wengine wanao unda kundi hilo kuwa ni Frank Mzambwe pamoja na Seif Shabani ambapo alisema kuwa
wanataraji kushirikisha nyota wa muziki wa kizazi kipya kama Banana Zoro na Maua Sami katika baadhi ya nyimbo zijazo.
Comments