Dr Edmund Mndolwa :Wizi ama ubadhilifu wa mali za chama katika uongozi wake kwa sasa litabaki historia
MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dr Edmund Mndolwa amesema utekelezaji
wake katika majukumu ya uongozi suala la wizi ama ubadhilifu wa mali za chama katika uongozi wake kwa sasa litabaki historia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Edmund Benard Mndolwa
Kamati iliyoundwa na Rais Magufuli kukagua mali za chama hicho, hivi karibuni ilifanyia kazi kwa miezi mitano na kufanikiwa kukusanya taafa za kuhakiki na kuchambua taarifa na nyaraka zenye maelezo kuhusu idadi, aina na hali ya mali zinazomilikiwa na kusimamiwa na chama hicho.
Akizungumza Dar es Salaam mwenyekiti huyo msomi Dk.Mdolwa katika kikao cha utekelezaji cha jumuiya ya wazazi ambacho
kinadaiwa kuwa cha dharula alisema kuwa anazifahamu changamoto zilizopo na kuwa uongozi wake huko imara.
"Kuhusiana na usimamizi wa mali za CCM mali za chama zitasimamiwa barabara kwa maslahi ya chama yaye mambo ya ukosefu wa maadili au matumizi mabaya ya ofisi katika utawala wangu yatabaki kama ndoto kwani ni lazima nijitume na kuwatumikia watanzania ili kutimiza ilani ya chama tawala(CCM),"Alisema Dkt.Mndolwa.
Alisema baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)imesema kuwa Agosti 12 mwaka huu itakuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Buyungu na wa madiwani katika kata 79
Tanzania Bara CCM tayari imejiandaa kushinda .
Dk.Mdolwa alichaguliwa kuwa mwenyekiti baada ya mwenyekiti wa zamani wa Jumuia hiyo,Alhaj Abdallah Bulembo ambaye kuelekea uchaguzi huo Desemba 2017 aliyeng'antuka baada ya kuongoza kwa miaka mitano.
Dkt.Mndolwa alisema wamejiandaa kushinda kwa kishindo kata zote 79 zinazotarajiwa kufanya uchaguzi mdogo mapema mwaka huu nakuwa wanajivunia maliasili watu katika ushindi huo.
Mwenyekiti huyo alisema CCM ni chama kikubwa sana nakuwa kinauwezo katika rasilimalizake hata wapinzani wanatambua na sasa wao kama viongozi na wanachama kwa sasa wamejipanga vizuri sana na kuwa wanamikakati ya kutosha na rasilimali watu .
Comments