Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jafo ameitaka Manispaa ya Ilala kusimamia vema zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara wa soko la Kisutu kupisha ujenzi wa soko la kisasa linalotarajiwa kuanza kujengwa Mwezi huu.
Akizungumza na wafanyabiashara wa soko hilo Jafo ameipongeza Manispaa ya Ilala kukamilisha kwa wakati ujenzi wa soko la muda litalotumiwa na wafanyabiashara wanaopisha ujenzi wa soko jipya.
Jafo pia ameitaka Manispaa hiyo kuhakikisha wafanyabiashara wote wasoko hilo kuandikishwa ili Kuzuia udanganyifu wa kuingiza wafanyabiashara wapya nakuwakosesha maeneo ambao wapo sasa.
"Katika Manispaa zote zenye miradi ya mpango mkakati nilizopita Ilala mme kuwa wakwanza kutekeleza kwa vitendo maandalizi na ujenzi wa soko, ila nisema jambo hili, hakikisheni wafanyabishara waliopo humu wanapewa kipaumbele watakapo Panga wote nafasi zitakazo baki a ndo wapewe Wafanya biashara wapya"alisema
Aidha ameagiza Mamalishe kupewa maeneo maalumu ya kufanya biashara zao ili wasisumbuliwe,huku akiagana apewe orodha ya Wafanyabiasha waliopo sasa ili aweze kufuatilia watakapo kuwa wa narudi sokojipya .
Pamoja na hayo Jafo amitaka manispaa ya Ilala kuweka sakafu katika Soko la muda, kuweka umeme na kujenga meza ili wafanyabishara wafanye biashara zao katika mazingira safi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema amemkikishia Mhe. Waziri kuwa zoezi hilo litafanyika kwa haki na kwamba yeye mwenyewe atasimamia ili kuhakikisha hakuna anaye one wa na kupoteza haki yake.
"Baada ya wiki mbili nita rudi tena hapa ili tuanze kuwapanga katika meza kila mmoja atapata eneo kutokana na nafasi iliyopo" alisema.
Kwaupande wao wafanyabiashara wa soko hilo wameshukuru Waziri Jafo kwa kufuatilia ujenzi huo na kupongeza Manispaa ya Ilala kwa mpango mzuri wa kuhakikisha wanafanya fanya biashara wote wenye maeneo katika Soko la Kisutu wa narudi katika maeneo yao baada ya ujenzi wa Soko.
Soko la kisasa la Kisutu litakuwa maghorofa nne na ujenzi unatarajiwa kuanza Mwezi huu, ambapo ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18, na litajengwa kwa thamani ya shilingi billion 13 na kampuni ya ujenzi ya Mohamedi Builders.
Comments