Skip to main content

Kesi ya Viongozi Chadema yasogezwa mbele

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri anatarajia kutoa uamuzi katika kesi inayowakabili viongozi 9 wa Chadema, July  10,2018 kama ajitoe kusikiliza kesi hiyo ama lah.
Hatua hiyo inatokana na viongozi akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe kuwasilisha hoja za kutaka Hakimu huyo ajitoe kwa sababu hawana imani naye.
Miongini mwa hoja ya Mbowe amedai ni adhabu tosha kwa upande wao kuripoti kituo cha Polisi cha Kati kila Ijumaa.

"Kwa miezi 3 kila siku ya Ijumaa tunakwenda kuripoti hiyo ni adhabu tosha ukizingatia sisi ni viongozi wa umma,"amedai.
Amedai kuwa kundi lao wote ni viongozi na wanatokea sehemu mbalimbali na wanamajukumu katika maeneo wanayitokea.
Pia amedai kuwa wanakosa haki za msingi kwa sababu mawakili wao wamekuwa wakipingwa wazi wazi pindi wanapowasilisha pingamizi zao.
Akifafanua zaidi, Mbowe alidai mwenendo wa hakimu wa kutokuthamini haki za msingi za watuhumiwa, kwamba aliuguliwa na kufiwa lakini hakuruhusiwa ombi la kumaliza msiba aliamriwa kurudi kusikiliza kesi na aliacha kumaliza msiba, anaonyesha ukali na hasira mawakili wa utetezi  wanapowasilisha hoja zao.  
Kutokana na hoja hizo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi July 5,2018 ili kutoa hatma yake kama aendelee kusikiliza kesi hiyo ama lah.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.
Pia wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee,   Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na Mbunge wa Tarime mjini, Esther Matiko.
Inadaiwa kuwa washitakiwa walitenda makosa hayo Februari 16, mwaka huu katika maeneo ya Viwanja vya Buibui, Mwananyamala na  barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni.
Wanadaiwa kuwa Februari 16,mwaka huu katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washitakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.
Inadaiwa kitendo cha kugoma  kulisababisha hofu iliyochangia  kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline na majeruhi kwa askari wawili ambao ni  H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...