Skip to main content

Soma hapa kongamano lililo andaliwa na UONGOZI Institute

SERIKALI ya awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuhakikisha kuwa hadi kufikia
mwaka 2025 Tanzania inakuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia maendeleo ya viwanda,
dhamira hiyo imeelezwa inasimamiwa kwa dhati na kwa vitendo na Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Picha inayohusiana
Hivyo imesisitizwa kuwa watanzania wanapaswa kumuunga mkono na kumsaidia katika
kutimiza dhamira hiyo njema kwa Taifa ambapo Tanzania imepitia hatua mbalimbali
za ujenzi wa viwanda, kabla na baada ya uhuru,kila awamu katika mchakato huo
ilipitia changamoto mbalimbali na kupiga hatua kwa kiasi fulani.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam jana katika ukumbi wa MWL.Julius Nyerere 
wakati wa Kongamano la “Wajibu wa Mashirika ya Umma katika Utekelezaji wa Ajenda ya
Tanzania ya Viwanda” lililoandaliwa na taasisi ya UONGOZI Institute mbapo hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt.Philip
Mpango akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Majaliwa
Kassim Majaliwa kwenye ufunguzi huo .


Alisema Serikali inaamini kuwa,Mashirika ya Umma yana mchango mkubwa katika kutimiza
azma hiyo na hivyo, ni imani yake kuwa lengo la ushiriki  katika Kongamano hilo ni
kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutimiza azma yake.


"Nisingelipenda kupitia historia ndefu ya ujenzi wa viwanda nchini;itoshe tu kusema
kuwa kila awamu katika mchakato huu ilipitia changamoto mbalimbali na kupiga hatua
kwa kiasi fulani. Kutokana na uzoefu uliopatikana katika mchakato huu,katika miaka
ya 1990, Serikali ilifanya marekebisho makubwa katika sera za uchumi wa nchi yetu 
Yako maeneo mengi yaliyofanyiwa maboresho,lakini katika muktadha wa maendeleo
ya viwanda nitataja manne,"alisema Mpango.


Alisema kwanza, Serikali ilitoa nafasi kwa soko kuwa chombo cha kugawa rasilimali(the
market was given more prominance in resource allocation) na; pili, sekta binafsi
ilipewa nafasi kuwa mbia muhimu wa maendeleo.

Aidha marekebisho ya Mifumo ya Kodi yalifanyika ili kuchochea shughuli za maendeleo na
viwanda. Vilevile, katika kipindi hicho,Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda(Sustainable
Industrial Development Policy -SIDP)ilitungwa ikiainisha,pamoja na mambo mengine,majukumu
ya Mashirika ya Umma na Sekta binafsi katika maendeleo ya viwanda,kwa ujumla marekebisho
hayo,yalisaidia katika ukuaji wa viwanda,ingawa si kwa kiwango kilichokusudiwa. 


Alisema katika kipindi cha mwaka 2005-2015,sekta ya viwanda imechangia kati ya asilimia 5
hadi 11 kwenye pato la Taifa au wastani wa asilimia 9 kwa kipindi hicho,pia,mchango wake
katika mauzo ya nje yaliongezeka kutoka asilimia 17 mwaka 2012 hadi asilimia 23 mwaka
2014; na kupungua hadi asilimia 19.1 mwaka 2015/16,mchango huo ni mzuri japo bado
hauridhishi,ndio maana katika mipango yetu ya sasa, tumedhamiria kuwa mchango wa
sekta ya viwanda kwenye pato la Taifa uongezeke kwa zaidi ya asilimia 10 kwa mwaka
na; katika mauzo ya nje uongezeke hadi kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2020.

"Kwa kuzingatia malengo niliyotaja Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele cha
kwanza kwa maendeleo ya viwanda. Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17
-2020/21) umeweka msisitizo mkubwa katika ustawishaji wa viwanda kama chombo cha
mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Mpango umeainisha maeneo ya kuzingatia
na mahitaji ya kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na yenye ustawi
katika maisha ya watu. Aidha, mpango unalenga kutekeleza Dira ya Maendeleo ya
Tanzania 2025 (Tanzania Development Vision 2025) inayolenga kuifanya Tanzania
kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,"alisema Waziri huyo.


Mpango alisema dahamira ya serikali kuendeleza agenda ya viwanda Serikali imetamka
bayana kuwa ujenzi wa uchumi wa viwanda ni ajenda namba moja na imetengeneza mikakati
inayotekelezeka ya kuelekea huko. Pili, Serikali imeamua kufufua viwanda vilivyobinafsi
shwa ambavyo vilikuwa vimekufa au kutofanya kazi. Tatu, Serikali imeamua kuchukua
viwanda ambavyo wawekezaji wake wameshindwa kuviendeleza na kuwakabidhi wawekezaji
wenye uwezo na nia ya kuvifufua na kuviendeleza.


Alisema uhakika zaidi ya hayo,Serikali imekusudia kuimarisha nidhamu katika utendaji
wa kazi,kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma,kuimarisha ukusanyaji wa mapato na
kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji,ikiwa pamoja na kutoa ahueni za kikodi kwa waweke
zaji katika viwanda vya ndani na kuanza utekelezaji wa mpango wa kuboresha mfumo wa
udhibiti wa biashara Tanzania ( BluePrint Regulatory Reforms to Improve the Business
Environment for Tanzania).


Hata hivyo Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazokabili Mashirika ya Umma,
zikiwemo za kisheria, kisera na kiutendaji pamoja na kuangalia namna bora ya kuchangia
katika ujenzi wa viwanda na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2025,maazimio ya Kongamano
hilo yataisaidia Serikali katika kufanya maboresho ya sheria,sera,mipango na mikakati
yake ya kuyafanya Mashirika ya Umma kuwa chachu ya maendeleo ya viwanda nchini.


Vilevile,Ili kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa viwanda,yeye kama Waziri ameshauri
Mashirika yote ya Umma yafanye jitihada za kujifunza kutoka katika Mashirika ya nchi nyingine kama
India,China na kwingineko zilizojenga uchumi wa viwanda kupitia mchango wa Mashirika
ya Umma yajifunze kwa namna gani Mashirika ya nchi hizo yalichangia na kufanya mageuzi
makubwa ya kiuchumi nchini mwao nakuwa amewapongeza waandaaji wa Kongamano hilo kwa
kumleta mtaalamu katika eneo hilo.


Alisema kuwa nimatumaini wasilisho lake katika majadiliano yaliyofanyika vitawajengea
uelewa wa namna gani mashirika ya nchi zilizoendelea katika viwanda yalichangia katika
maendeleo yao.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Mwana muziki Marufu kwa jina la Chuck Brown Afariki Dunia Akiwa na umri wa miaka 75

View Photo Gallery — Chuck Brown dies at 75: The “godfather of go-go” has died By Chris Richards, Updated: Wednesday, May 16, 4:42 PM Chuck Brown, the gravelly voiced bandleader who capitalized on funk’s percussive pulse to create go-go, the genre of music that has soundtracked life in black Washington for more than three decades, died May 16 at the Johns Hopkins University hospital in Baltimore. He was 75. The death, from complications from sepsis, was confirmed by his manager, Tom Goldfogle. Mr. Brown had been hospitalized for pneumonia. Known as the “Godfather of Go-Go,” the performer, singer, guitarist and songwriter developed his commanding brand of funk in the mid-1970s to compete with the dominance of disco. Like a DJ blending records, Mr. Brown used nonstop percussion to stitch songs together and keep the crowd on the dance floor, resulting in marathon performances that went deep into the night. Mr. Brown said the style got its name because “the music j...