Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa Agosti 12 mwaka huu itakuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Buyungu na wa madiwani katika kata 79 Tanzania Bara.
Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji Semistocles Kaijage ameeleza hayo hivi karibuni jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wajumbe wa tume hiyo pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini ambapo amesema wameshaandaa ratiba ya uchaguzi huo na wanatarajia form kuanza kuchukuliwa Julai 8 hadi 14 mwaka huu.
Comments